|
Baraza kuu la 59 la Umoja wa Mataifa jana lilifanya mkutano maalum kukumbuka miaka 60 tangu kukombolewa kwa kambi ya Auscgwitz. Hii ni mara ya kwanza kwa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kufanya mkutano maalum kuhusu tukio hilo, mkutano ambao umeanzisha shughuli za kuadhimisha miaka 60 tangu upate ushindi katika vita vya kupambana na ufashisti duniani.
Wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia, Ujerumani ya nazi iliwaua wayahudi karibu milioni 6. Kambi ya Auscgwitz iliyokuwepo kusini mwa Poland pia iliitwa kuwa kambi ya vifo, ambayo ilikuwa ni kambi kubwa kabisa iliyojengwa na Ujerumani ya nazi wakati huo. Katika miaka mitano toka mwaka 1940 hadi 1945, wayahudi zaidi ya milioni moja wa nchi zaidi ya 20 za Ulaya waliuawa kishenzi katika kambi hiyo, wakiwemo kina mama na watoto wengi. Tarehe 27 Januari mwaka 1945, Jeshi jekundu la Urusi lilikomboa kambi ya Auscgwitz na kuwaokoa watu 7000 walionusurika mauaji kwenye kambi hiyo.
Wakati mkutano wa kukumbuka miaka 60 tangu kukombolewa kwa kambi ya Auscgwitz ulipoanza, watu wote waliohudhuria mkutano huo walisimama wima na kukaa kimya kwa dakika moja kuwaomboleza wayahudi milioni 6 waliouawa na wanazi katika vita vikuu vya pili vya dunia. Watu walionusurika katika mauaji kwenye kambi ya Auscgwitz, watu waliopewa tuzo ya Nobel na mawaziri wa mambo ya nje au wajumbe wa nchi husika walitoa hotuba kwenye mkutano huo.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Kofi Annan alipotoa hotuba ya ufunguzi aliitaka jumuiya ya kimataifa ichukue tahadhari zaidi kwa vitendo vya kupinga wayahudi na ubaguzi rangi wa aina nyingine, na kuchukua hatua halisi kuzuia matukio ya huzuni kama mauaji ya nazi yasitokee tena. Alisema kuwa, Umoja wa Mataifa kamwe haupaswi kusahaua kuwa Umoja wa Mataifa ulianzishwa kwa kulenga kupambana pigo unazi, na ni ugaidi wa mauaji makubwa ya nazi uliohimiza jumuiya ya kimataifa kuweka wazi jukumu la Umoja wa Mataifa kwenye "Katiba ya Umoja wa Mataifa". Bwana Annan aliainisha pia kuwa, jumuiya ya kimataifa pia inapaswa kuwajibika hivyo hivyo kwa mataifa mengine ambayo huenda yatapata ajali kama walivyoipata binadamu wayahudi. Matukio mengi ya kuwaogopesha watu ya kupoteza ubinadamu yanatokea katika dunia ya sasa, jumuiya ya kimataifa haipaswi kupuuza matukio hayo, hata kukataa kuona kuwepo kwa matukio hayo.
Mwaka huu si kama tu ni mwaka wa 60 tangu kupata ushindi katika vita vya kupambana na ufashisti, bali pia ni mwaka wa 60 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa. Umoja wa Mataifa uliopita vipengele vingi katika miaka 60 iliyopita unakabiliwa na changamoto kubwa ambazo hazikutokea hapo awali. Kwanza, baada ya nchi za magharibi zinazoongozwa na Marekani na Uingereza kuanzisha vita dhidi ya Iraq bila idhini ya Umoja wa Mataifa, umuhimu wa Umoja wa Mataifa umeathiriwa vibaya; pili, kashfa iliyofichuliwa kuhusu mpango kuhusu mafuta ya Iraq kwa chakula imeufanya Umoja wa Mataifa kujitumbukiza kwenye hali taabani, hata Bwana Annan mwenyewe alikuwa katibu mkuu wa kwanza aliyedaiwa na wahafidhina wa Marekani katika historia ya Umoja wa Mataifa; tatu, baada ya kumalizika kwa vita vya baridi, kutokana na mabadiliko ya hali ya kimataifa, dosari mbalimbali ya uvimbe wa mashirika na ufanisi wa chini wa Umoja wa Mataifa yameonekana siku hadi siku, ambayo yameathiri vibaya heshima na umuhimu wa Umoja wa Mataifa.
Ndiyo maana, mkutano huo maalum umefanyika katika hali hiyo, ambao umeleta fursa nzuri kabisa kwa Umoja wa Mataifa kufufua heshima yake. Kikundi watu mashuhuri wanaoshughulikia suala la mageuzi ya Umoja wa Mataifa kimetoa ripoti ya mapendekezo kuhusu mageuzi ya Umoja wa Mataifa ili kuimarisha umuhimu wa Umoja wa Mataifa. Mapendekezo hayo na mkutano huo maalum vimeonesha kuwa Umoja wa Mataifa ni Jumuiya ya kimataifa ya kulinda amani na utulivu ambayo umuhimu wake hauwezi kuchukuliwa na Jumuiya nyingine yoyote.
Idhaa ya Kiswahili 2005-01-25
|