Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-25 15:23:03    
Serikali ya muda ya Iraq yaandaa uchaguzi mkuu katika hali ya ugaidi

cri
Hivi sasa, hali mbaya ya usalama bado ni changamoto kubwa inayoukabili uchaguzi mkuu wa Iraq. Tarehe 24, matukio mengi ya ugaidi yalitokea nchini Iraq. Matukio hayo kwa jumla yaliwaua watu watano na kuwajeruhi wengine 15. Kati ya watu hao, karibu wote ni polisi na askari wa kikosi cha usalama cha Iraq. Kundi la ugaidi linaloongozwa na kiongozi nambari tatu wa kundi la Al-Qaeda Abu Musab Al-Zarqawi lilitangaza kuhusika na matukio hayo.

Siku moja iliyopita, Al Zarqawi alitoa taarifa kwenye kituo cha tovuti akieleza kuanzisha vita dhidi ya uchaguzi mkuu wa Iraq. Taarifa hiyo inashutumu kuwa uchaguzi mkuu wa Iraq ni udanganyifu mtupu unaofanywa na wamarekani na kueleza kuwa demokrasia ya kimarekani iliyopendekezwa na Marekani na rafiki yake, kundi la Shia imehaini demokrasia ya kiislam. Siku hiyo, serikali ya muda ya Iraq ilitangaza kuwa polisi na kikosi cha usalama cha Iraq kiliwakamata wasaidizi waandamizi wawili wa Al Zarqawi, mmoja ni Abu Omar Al-Kurdi ambaye aliongoza kuzusha milipuko 30 mikubwa kwa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Iraq na ofisi ya waziri mkuu Iyad Alawi na mwingine ni kiongozi wa idara ya uenezi habari wa Al Zarqawi, Bw Mohsen Al-Duleimi.

Ili kukabiliana na matukio ya ugaidi yanayotokea kila wakati na kuleta mazingira yenye usalama, serikali ya muda ya Iraq hivi karibuni iliamua kuchukua hatua za usalama za kufunga mpaka na kudhibiti hali ya usalama sehemu sehemu, ili kuzuia nguvu zenye msimamo mkali za kigeni zisiingie nchini Iraq na kushirikiana na nguvu zenye msimamo mkali nchini Iraq. Hatua hizo zitakazotekelezwa katika kipindi cha uchaguzi mkuu ni pamoja na kufunga uwanja wa ndege wa Baghdad na vipito vyote barani kwa saa 48, kutekeleza sheria ya kutoruhusu watu kutoka nje wakati wa usiku, kupiga marufuku watu kuwasiliana kati ya mikoa mikubwa na kupiga marufuku ya kutembea na silaha na magari karibu yote barabarani.

Ingawa uchaguzi mkuu unatishiwa na matukio mbalimbali ya ugaidi, lakini kazi ya maandalizi ya uchaguzi huo inafanyika kwa juhudi, masanduku elfu 90 ya kura na karatasi za kupigia kura milioni kadhaa zimefikishwa nchini Iraq. Ili kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa halali, idara za uchaguzi za Iraq zimeunda kikosi cha kusimamia uchaguzi chenye watu zaidi ya elfu 12, wakiwemo wachunguzi 128 wa uchaguzi wa jumuiya mbalimbali za kimataifa.

Idhaa ya kiswahili 2005-01-25