Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-25 16:55:43    
India na Pakistan zapuuza kwa makusudi tukio la kukiuka mkataba wa kusimamisha vita

cri

Baada ya India kulaani mara mbili Pakistan kukiuka mkataba wa kusimamisha vita katika sehemu ya Kashmir wiki iliyopita, tarehe 24 Pakistan pia iliilaani India kwa kukiuka mkataba katika siku ya tarehe 21. Lakini wasemaji wa wizara za mambo ya nje za nchi mbili wote walikanusha kuwahi kulaaniana. Wachunguzi wanaona kuwa ingawa mkwaruzano kweli ulitokea katika sehemu ya Kashmir hivi karibuni, lakini  mkwruzano huo hautaathiri mazungumzo ya amani ya pande mbili.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan, Masood Khan kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 24 alisema kuwa tokea saa tisa hadi saa 12 alasiri tarehe 21 jeshi la India iliifyatulia risasi sehemu ya Kashmir upande wa Pakistan, lakini jeshi la Pakistan halikujibu, kwa hiyo hayakutokea madhara yoyote. Lakini msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya India ilikanusha kauli hiyo, alisema kuwa jeshi la Pakistan lilitaja tukio hilo katika mawasiliano ya simu na jeshi la India, kwamba upande wa India ulifanya uchunguzi, na unaona kuwa malalamiko ya Pakistan hayana msingi. Kabla ya hapo, tarehe 18 na 20, katika sehemu ya Kashmir upande wa India iliwahi kutokea tukio la kufyatua risasi mara mbili, India iliilaani Pakistan kwa kukiuka mkataba wa kusimamisha vita na kuharibu hali ya utulivu ya miezi 14, lakini Pakistan ilikana.

Mgogoro wa sehemu ya Kashmir kati ya India na Pakistan ni tatizo muhimu katika uhusiano wa nchi hizi mbili, na mgogoro huo umekuwepo kwa karibu miaka 60. Hadi hivi sasa watu zaidi ya elfu 60 wameuawa katika mgogoro huo, na wengi wao ni raia wa kawaida. Tarehe 11 mwaka 2003 nchi hizo mbili zilifikia mwafaka wa kusimamisha vita katika sehemu ya Kashmir, na pande mbili zilianza mazungumzo ya amani.

Baada ya tukio la kufyatua risasi kutokea, kwa kuwa wakati huo pande mbili zilikuwa zikifanya mazungumzo ya amani, ingawa zililaana, lakini pia zinawasiliana ili tukio lisiendelee kuwa baya. Tarehe 19 na 20 majeshi ya pande mbili yalijadiliana kuhusu Pakistan kukiuka mkataba wa kusimamisha vita, na Pakistan ilitaka India ifanye uchunguzi wa makini. Pande mbili zilikubaliana tukio kama hilo litatatuliwa kwa kufanya mazungumzo kati ya majeshi mawili. Jemadari mkuu wa India N.C.Vij tarehe 22 alipuuza kwa makusudi matukio ya kufyatua risasi yaliyotokea katika siku ya tarehe 18 na 20, akisema matukio hayo "si kitu". Shirika la Habari la Asia la India lilimnukuu Bw. Vij akionya kuwa haifai kutangaza habari kama hiyo kabla ya kufanya uchunguzi wa kina na kubaini ukweli. Aliona kuwa ilhali mkataba wa kusimamisha vita umeanza kutekelezwa, basi pande mbili lazima ziheshimu mkataba huo. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan Masood Khan tarehe 24 alisema kuwa hali ya kutokuweko vita katika muda wa miezi 14 ni fursa nzuri kwa pande mbili kujenga uaminifu, na pia alisema kuwa matukio ya kufyatua risasi yaliyotokea katika tarehe 18 na 20 yote yalitokea katika sehemu ya Kashmiri upande wa India, kwa hiyo India inapaswa kufanya uchunguzi na kufahamisha matokeo ya uchunguzi huo, na aliahidi kuwa Pakistan itaendelea kutekeleza mkataba wa kusimamisha vita, na India inapaswa kufanya vivyo hivyo.

Katika mahojiano na waandishi wa habari, Masood Khan alisema tukio la kufyatua risasi halitaathiri mchakato wa mazungumzo ya amani, na mazungumzo yatafanyika tokea mwezi wa nne hadi sita kama yalivyopangwa na mwezi wa saba mazungumzo ya makatibu wa wizara za mambo ya nje yatafanyika vile vile. Kadhalika, mawaziri wakuu wa nchi mbili watakutana katika mkutano wa kilele wa Nchi za Umoja wa Asia ya Kusini mwanzoni mwa mwezi ujao. Kisha waziri wa mambo ya nje wa India Natwar Singh atakuwa ziarani nchini Pakistan. Bw. Masood Khan alisema kuwa amani inanufaisha nchi zote mbili, na Pakistan itajitahidi kutatua mgogoro wa nchi mbili kwa njia ya mazungumzo.

Tokea mazungumzo ya amani yaanze mwanzoni mwa mwaka jana, pande mbili ziliwahi kufanya mazungumzo mara nyingi na uhusiano wa pande mbili umekuwa ahueni. Hata hivyo kutokana na kuwa matatizo kati ya nchi hizo mbili yamekuwa ya miaka mingi tena ya utatanishi, mazungumzo bado hayajapiga hatua kubwa, lakini serikali za nchi mbili zimewahi kueleza kuwa zitajitahidi kusukuma mazungumzo ili kupata amani ya kudumu ya kikanda. Katika mazingira mazuri kama hayo, wachambuzi wanaona kuwa tukio la kufyatua risasi ni dogo, ikiwa pande mbili zitavumilia machafuko makubwa hayatatokea katika sehemu ya Kashmir.

Idhaa ya kiswahili 2005-01-25