Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-25 21:07:21    
Addis Ababa-Mwaka 2004 watu 100,000 nchini Ethiopia walikufa kutokana na ukiwmi

cri

    Wizara ya afya ya Ethiopia jana ilitoa ripoti ikisema kuwa, mwaka 2004, watu 100,000 wa nchi hiyo walikufa kutokana na ugonjwa wa ukimwi.

    Ripoti hiyo ilitolewa na waziri wa afya wa Ethiopia kwenye mkutano wa kuzindua mpango wa kukinga na kudhibiti maambukizi ya ukimwi nchini humo. Ripoti ilisema kuwa mwaka jana, watu 115,000 wa nchi hiyo walikufa kutokana na ukimwi, kati ya hao 90,000 ni watu wazima na wengine 25,000 ni watoto. Pia kuna watu milioni 1.5 wenye virusi vya ukimwi, kati yao 95,000 ni watoto wenye umri chini ya miaka 15.

    Waziri mkuu wa Ethiopia Bwana Meles Zenawi alitoa mwito kwa wananchi wote washiriki katika harakati hiyo ya kupambana na ukiwmi, alisema kuwa, serikali itachukua hatua mwafaka kukinga na kudhibiti balaa hilo lisienee zaidi.