Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-26 15:44:58    
Uchumi wa China ulizidi 9.5% mwaka 2004

cri
    Uchumi wa China uliendelea kwa kasi na kwa hatua madhubuti mwaka 2004. Kutokana na mahesabu ya awali, thamani ya jumla ya uzalishaji ya China ilifikia RMB yuan trilioni 13.65, kiasi hicho kiliongezeka kwa asilimia 9.5 kuliko mwaka juzi.

    Mkuu wa Ofisi ya takwimu ya China Bw. Li Deshui alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 25 kwenye Ofisi ya habari ya Baraza la serikali ya China. Bw. Li alisema kuwa, mwaka 2004, chini ya uongozi sahihi wa Kamati kuu ya chama cha kikoministi na baraza la serikali ya China, idara za ngazi mbalimbali za China zimekuwa na wazo la kujipatia maendeleo kwa njia ya kisayansi, na kutekelea vitendoni kuimarisha na kukamilisha hatua za marekebisho na udhibiti wa uchumi, na kuzuia hali zinazoharibu maendeleo ya uchumi.

    Mwaka 2004, thamani ya uzalishaji wa shughuli zilizo za nguzo ya kwanza ya China kama vile kilimo, misitu, ufugaji na uvuvi iliongeza kwa asilimia 6.3 na kupata ongezeko la RMB yuan trilioni 2.07; thamani ya shughuli za nguzo ya pili zikiwemo uchimbaji wa madini, uzalishaji viwandani, uzalishaji wa umeme, gesi na maji na ujenzi iliongezeka kwa asilimia 11.1 na kupata ongezeko la RMB yuan trilioni 7.23, na thamani ya shughuli za nguzo ya tatu iliongezeka kwa asilimia 8.3 na kupata ongezeko la fedha RMB yuan trilioni 4.33. Shughuli za nguzo ya tatu zinahusu mawasiliano, huduma, biashara na nyinginezo.

    Ongezeko la uwekezaji vitega uchumi kwenye eneo la mali za zisizohamishika lilipungua kiasi, na mfumo wa uwekezaji vitega uchumi ulibadilika. Mwaka 2004, uwekezaji vitega uchumi kwenye mali zisizohamishika ulifikia RMB yuan trilioni 7, kiasi hicho kiliongezeka kwa asilimia 25.8 kuliko mwaka juzi, lakini ongezeko hilo lilipungua kwa asilimia 1.9. Uwekezaji wa vitega uchumi kwenye shughuli za nguzo ya kwanza ya China uliongezeka kwa asilimia 20.3, na ongezeko la uwekezaji vitega uchumi kwenye viwanda kadhaa vilivyopata maendeleo ya kasi kupita kiasi ulipungua kwa kiasi kikubwa.

    Bei za vitu masokoni kwa mwaka 2004ziliongezeka. Thamani ya jumla ya mauzo ya rejareja ilifikia RMB yuan trilioni 5.39, na kiasi hicho kiliongezeka kwa asilimia 10.2, na kasi ya ongezeko hilo iliongezeka kwa asilimia 1 kuliko mwaka juzi. Bei ya matumizi ya wananchi ya mwaka jana iliongezeka kwa asilimia 3.9, na ongezeko lake liliinuka kwa asilimia 2.7 kuliko mwaka juzi.

    Uchumi na biashara ya nje ulipata maendeleo ya kasi. Thamani ya jumla ya biashara ya kimataifa ilifikia dola za kimarekani trilioni 1.15, na kupata ongezeko la asilimia 35.7. Kati ya hizo thamani ya bidhaa nje iliongezeka kwa asilimia 35.4, na bidhaa zilizoagizwa kutoka nchi za nje zilipata ongezeko la asilimai 36. Urari mzuri wa biashara ulifikia dola za kimarekani bilioni 32, na kuongezeka kwa dola za kimarekani bilioni 6.5 kuliko mwaka juzi. Matumizi ya mitaji ya nje yalifikia dola za kimarekani bilioni 60.6, kiasi ambacho kiliongezeka kwa asilimia 13.3.

    Bw. Li Deshui alipohojiwa alisema kuwa, inapaswa kuzingatia zaidi matatizo kwenye uendeshaji wa uchumi. Hivi sasa, suala muhimu ni kuzuia kurudi nyuma kwa uwekezaji wa vitega uchumi kwenye mali zisizohamishika.

    Bw. Li anaona kuwa, mazingira ya maendeleo ya uchumi kwa mwaka 2005 ni mazuri, na maendeleo ya uchumi wa taifa yanatazamiwa kudumisha maendeleo ya kasi ikiwa hatua mbalimbali za marekebisho na udhibiti wa jumla wa uchumi zitaimarishwa na kukamilishwa vizuri.

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-26