Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-26 16:37:30    
Supu yenye ladha ya siki na pilipili

cri

Mahitaji

Doufu gramu 30, uyoga mweusi gramu 20, slesi zilizokaushwa za vichipukizi vya mianzi gramu 50, vipande vya nyama ya nguruwe gramu 50, vitunguu maji gramu 5, tangawizi gramu 5, yai 1, maji bakuli 2, mchuzi wa soya kijiko 1, siki vijiko 2, chumvi kijiko 1, M.S.G nusu kijiko, unga wa pilipili manga nusu kijiko, maji ya wanga vijiko 2, kiasi kidogo cha mafuta ya uto na mvinyo wa kupikia

Njia

1. kata doufu, uyoga mweusi na slesi zilizokaushwa za vichipukizi vya mianzi, vitunguu maji, tangawizi ziwe vipande vipande, tia vipande vya nyama ya nguruwe ndani ya bakuli moja na tia mchuzi wa soya, maji ya wanga na mvinyo wa kupika halafu kuikoroga. Koroga yai. Tia pilipili manga na vitunguu maji, tangawizi katika bakuli kubwa.

2. pika vipande vya nyama ya nguruwe halafu ipakue. Chemsha maji, tia vipande vya nyama ya nguruwe, doufu, uyoga mweusi na slesi zilizokaushwa za vichipukizi ya mianzi, halafu tia mchuzi wa soya, mvinyo wa kupika, maji yaliyochemshwa tia M.S.G, chumvi, siki, maji ya wanga, punguza moto kidogo na tia yai, koroga, pakua katika bakulini na andaa.