Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-27 15:45:14    
Uchaguzi mkuu wa Iraq watarajiwa kufanyika bila vikwazo

cri

Baada ya siku chache zijazo, yaani tarehe 30 mwezi Januari, Iraq itafanya uchaguzi mkuu wa kwanza tangu Marekani ilipoanzisha vita vya Iraq. Hilo ni jambo kubwa katika mchakato wa mpito wa kisiasa nchini Iraq ambalo linafuatiliwa sana na watu wa sekta mbalimbali nchini Iraq na wa nchi za nje. Watu wanatumai kuwa katika hali yenye migogoro ya hivi sasa, uchaguzi mkuu wa Iraq utaweza kufanyika tarehe iliyopangwa na bila vikwazo na kuleta mazingira kwa ukarabati wa kisiasa na kiuchumi nchini humo.

Kutokana na katiba ya taifa ya muda iliyopitishwa mwaka jana, uchaguzi huo utachagua bunge la mpito lenye wabunge 275 ambalo litaunda serikali ya mpito na kutunga katiba ya taifa ya kudumu, ili kuweka msingi kwa ajili ya kuchagua bunge rasmi na kuunda serikali rasmi mwishoni mwa mwaka kesho. Kwa hiyo, uchaguzi mkuu huo sio tu utakuwa muhimu kwa ajili ya kuendeleza mchakato wa ukarabati wa kisiasa wa Iraq, bali pia kwa ajili ya kutimiza lengo la Wairaq waitawale Iraq haraka iwezekanavyo, na kutimiza utulivu wa kudumu nchini humo.

Kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika bila vikwazo, ni maoni ya pamoja ya vyama vikuu nchini Iraq. Rais Ghazi Al-Yawar wa serikali ya muda ya Iraq, makamu wake Rowsch N. Shaways na waziri mkuu Iyad Allawi wote wanatumai kuwa uchaguzi mkuu utafanyika katika tarehe iliyopangwa. Uchaguzi mkuu huo pia unaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan aliwataka Wairaq washiriki katika uchaguzi huo, akisema kuwa ingawa hali ya nchini Iraq sio ya kuridhisha, lakini Wairaq wengi wanataka kupiga kura na kutumia haki zao.

Tatizo muhimu linaloathiri uchaguzi mkuu ni shughuli mbalimbali za ugaidi. Watu wenye silaha wa makundi mbalimbali nchini Iraq wamefululiza kuanzisha mashambulizi na kujaribu kuharibu uchaguzi mkuu. Katika hali hiyo, wapiga kura wataweza kupiga kura kwa uhuru na haki au la, ni jambo la kuwatia watu wasiwasi. Zaidi ya hayo, jambo ambalo vyama vikuu vya Waislam wa madhehebu ya Sunni vinasusia uchaguzi huo pia limewatia watu mashaka kama matokeo ya uchaguzi huo yatakuwa na uwakilishi mkubwa.

Watu wameona kuwa mambo mwafaka yameleta matumaini kwa mafanikio ya uchaguzi mkuu, kwamba ili kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika bila vikwazo, serikali ya muda wa Iraq imechukua hatua kali mfululizo za ulinzi. Waziri mkuu Iyad Allawi alisema kuwa serikali yake inaweza kuhakikisha usalama katika vituo vya upigaji kura na wapiga kura wataweza kupiga kura bila wasiwasi. Waziri wa mambo ya taifa wa serikali ya muda Bw. Wael Abdul Latif pia alisema kuwa hali ni ya utulivu katika mikoa 14 kati ya mikoa 18 yote nchini Iraq.

Inapaswa kuainisha kuwa chanzo kikuu cha kusababisha hali ya migogoro kwa hivi sasa ni ukaliaji wa jeshi la muungano la nchi nyingi likiongozwa na Marekani nchini Iraq. Mapambano ya watu wenye silaha kupambana na Marekani hayataisha kabla ya ukaliaji huo kumalizika. Kwa upande mwingine, mashambulizi ya ugaidi yameongeza misiba kwa wairaq na raia wamekuwa wanadhulumiwa sana. Kwa hiyo jambo muhimu la kutatua mgogoro wa Iraq ni kumaliza kabisa ukaliaji wa jeshi la muungano wa nchi nyingi na kurejesha haki ya wairaq ya kuwa mabwana wa taifa. Uchaguzi mkuu huo ni hatua muhimu itakayopigwa kuelekea lengo hilo.

Idhaa ya kiswahili 2005-01-27