Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-27 18:40:57    
Mpango wa kueneza elimu ya afya nchini China

cri
    Ili kuhimiza jamii yote kushirikiana katika kuzuia mwelekeo 011 wa kuongezeka kwa magonjwa sugu nchini China, "Mpango wa kueneza elimu ya afya nchini China" unaoendeshwa kwa pamoja na Ofisi ya Udhibiti wa Maradhi na Ofisi ya Habari za Wizara ya Afya, na Shirikisho la Waandishi wa Habari la China umeanzishwa hivi karibuni hapa Beijing.

    Katika miaka ya karibuni, magonjwa sugu mbalimbali yanaongezeka kwa kasi nchini China, kati yao wagonjwa wa shinikizo la damu na shahamu nyingi za damu wamefikia milioni 160, na wagonjwa wa kisukari na wanene wa kupita kiasi pia wanaongezeka kwa haraka. Hatua kimsingi ya kuzuia kueneza kwa magonjwa hayo sugu ni kutilia mkazo kueneza elimu ya afya kwa wananchi wote.

    Mpango wa kueneza wa elimu ya afya ya China unayoungwa mkono na serikali na watu wa sekta mbalimbali nchini China unatoa fursa nzuri kufahamisha elimu ya kujipatia afya kwa wananchi wote, na kila mwaka unapanga kufanya harakati ya kueneza elimu ya ugonjwa moja sugu unaotishia afya ya watu. Harakati hizo zitafanyika kwa ajili ya raia, wagonjwa, waandishi wa habari na madaktari. Mwaka 2005, mpango huo utaweka mkazo kutangaza elimu kuhusu ugonjwa wa shinikio la damu ambao ni wa kwanza kuhatarisha afya nchini China.

    Mpango huo wa mwaka huu-(Shinikizo la damu-2005), umepata misaada ya fedha ya Kampuni ya dawa ya Hui Rui, na utatekelezwa kwa hatua tatu pamoja na kusambaza bure vitabu vya mwongozo kuhusu kinga na tiba ya ugonjwa wa shinikizo la damu kwa waandishi wa habari, kuanzisha shindano kuhusu elimu ya kuzuia shinikizo la damu mwaka 2005, na kuchagua makala ya magonjwa milioni 160 wa shinikio la damu kuhusu walivojitahidi kuzuia ugonjwa wao, na kubadilishana uzoefu kuhusu ugonjwa huo kati ya waandishi wa habari na madaktari kwa muda unaopangwa.

    Kwenye sherehe ya kuanzishwa kwa harakati hiyo, vitabu vya mwongozo 5000 vilivyoandaliwa na Ofisi ya Udhibiti wa Maradhi ya Wizara ya Afya vilisambazwa bure kwa waandishi wa habari na watu wanaoshughulikia ripoti kuhusu afya na matibabu. Wakati huo huo, waendeshaji wa mpango huo pia walianzisha harakati ya shindano la elimu ya afya nchini China (shinikizo la damu 2005), na waandishi wa habari wanaoshughulikia ripoti ya afya na matibabu, wagonjwa wa shinikizo la damu, madaktari na waandishi wa elimu ya kisayansi wanakaribishwa kuandika makala na kushiriki kwenye shindano hilo. Uchaguzi huo utaweka tuzo tatu zikiwemo tuzo ya kueneza elimu ya ugonjwa wa shinikizo la damu, Tuzo ya ripoti bora kuhusu shinikizo la damu, na Tuzoa makala ya wagonjwa wa shinikizo la damu.

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-27