Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-27 20:07:29    
Mji wa Shanghai

cri

    Mji wa Shanghai unaitwa Hu kwa kifupi, na pia unaitwa Shen. Inasemekana kuwa katika Enzi ya Madola ya Kivita, sehemu hiyo ilikuwa sehemu iliyotawaliwa na Dola la Chu.

    Katika karne ya 16 yaani katikati ya Enzi ya Ming, mji wa Shanghai ulikuwa kituo cha utengenezaji wa vitambaa vya pamba nchini China. Mwaka 1685 katika Enzi ya Qing, forodha ya Shanghai ilianzishwa. Wakati huo Shanghai ulikuwa mji wenye wakazi laki 2. Baada ya vita vya kasumba, Shanghai ilikuwa bandari muhimu ya biashara na nchi za nje. Baadaye nchi za magharibi zilivamia Shanghai na kuufanya mji huo kuwa mji wa nusu kimwinyi na nusu kikoloni. Tarehe 27 mwezi Mei mwaka 1949, mji wa Shanghai ulikombolewa.

    Ukombozi ulifungua ukurasa mpya katika historia ya maendeleo ya Shanghai. Watu wa Shanghai wakiongozwa na Chama cha Kikomunisti cha China walifanya kazi kwa bidii kwa miaka 50 na kubadilisha kabisa hali ya zamani ya Shanghai ya nusu kikoloni na nusu kimwinyi, na sura ya kiuchumi na jamii imepata mabadiliko makubwa. Hasa baada ya China kuanza kutekeleza siasa ya mageuzi na ufunguaji mlango mwaka 1978, sekta mbalimbali za uchumi na jamii za Shanghai zimepata mageuzi makubwa, na nguvu ya jumla ya mji huo imeongezeka kwa kiasi kikubwa, sura yake inaboreshwa siku baada ya siku. Shanghai kimekuwa kituo kikubwa kabisa cha kiuchumi na mji maarufu wa kihistoria na kiutamaduni nchini China, na mji huo utakuwa moja ya vituo vya kiuchumi, kifedha, kibiashara na usafarishaji duniaini.

    Mji wa Shanghai uko katika latitudo ya kaskazini digrii 31'14" na longitudo ya mashariki digrii 121'29". Uko katika Delta ya Mto Changjiang, na katika upande wa mashariki unapakana na Bahari ya Mashariki, kusini unapakana na ghuba ya Hangzhou, magharibi unapakana na mkoa wa Jiangsu na mkoa wa Zhejiang na kaskazini ni Mto wa Changjiang. Uko katikati ya ukanda wa pwani wa China na ni bandari nzuri ya mto na bahari.

    Hali ya hewa ya Shanghai ni hali ya hewa ya pepo za msimu za ukanda wa nusu tropiki wa kaskazini. Katika sehemu hiyo kuna majira manne na mvua nyingi. Hali ya hewa ni ya fufutende. Majira ya spring na ya autumn ni mafupi, na majira ya baridi na ya joto ni marefu. Joto la wastani la mwaka mzima ni centigrade nyuzi 17.7. Asilimia 70 ya mvua inanyesha katika kipindi cha mwezi Mei hadi mwezi Septemba.

    Mji wa Shanghai una mito na maziwa mengi. Hivyo maliasili ya maji ni nyingi. Eneo la maji mjini humo ni kilomita za mraba 697 ambalo limechukua asilimia 11 ya eneo la mji huo. Mito mingi mjini humo ni matawi ya Mto Huangpujiang. Mto huo ambao chanzo chake ni Ziwa Taihu una urefu wa kilomita 113. Maji ya mto huo mkubwa wenye kina kirefu hayagandi mwaka mzima, hivyo mto huo ni njia muhimu ya usafirishaji mjini Shanghai.

  

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-27