Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-28 19:20:58    
Uchongaji Kwenye maganda ya Mayai

cri

    Tangu zamani hadi siku hizi ufundi wa uchongaji nchini China uko wa aina tatu: uchongaji mgumu, na uchongaji kwenye vitu vidogo kabisa. Uchongaji kwenye mayai ni wa aina ya uchongaji wa juu ya vitu vilivyo vyepesi vya kuvunjika.

    Wasanii huchonga picha nzuri na za ajabu juu ya maganda ya mayai ya kuku, bata, bata-bukini na jiwe la kaburi lenye unene wa chini ya milimita 0.5 tu.

    Chen Fusheng wa Wilaya ya Dongan jimboni Hunan alijifunza utaalam wa kuchonga tangu akiwa mtoto. Akivutiwa na uchoraji wa kwenye mayai, alianza kufanya utafiti wa sanaa ya uchongaji wa kwenye mayai. Ingawa mara nyingi alishindwa mara nyingi, lakini alidhibiti hatua kwa hatua hulka za kila aina ya maganda ya mayai kuhusu unene, ugumu na ufikichikaji wake na akaweza kuchonga mabombwe mbalimbali kwa kisu juu ya maganda hayo, nayo ni pamoja na milima, mito, maua, ndege, binadamu na hata mashairi. Mpaka sasa Chen Fusheng amekwishadhibiti ustadi wa uchongaji wa mbinuko, wa mbonyeo , wa matabaka kadhaa na uchongaji wa kukomba. Maumbo ya michongo yake, yako ya aina kadhaa wa kadhaa, kama vile yai moja, mayai kadhaa yaliyounganishwa pamoja na picha zilizotengenezwa kwa kubandikwa kiustadi kwenye maganda ya mayai vilivyochongwa.

    Maganda ya mayai yaliyochongwa ni vigumu kuwasilishwa na maumbo yake bado ni machache, hata hiyo yamekwishakuwa ua moja dogo kwenye uwanja wa sanaa za uchongaji.

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-27