Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-28 19:20:39    
Kitambaa cha Kiunoni

cri

     Katika makala hii, nitawaeleza kuhusu kitambaa cha kiunoni kilichotariziwa na kinachotumiwa kujifunga kiunoni na wanawake wa Kabila la Wabai, wanaoishi kwenye milima mirefu ya kando ya Mto Nujiang, magharibi ya Jimbo la Yunnan.

     Aina, ukubwa na tarizi za kutambaa cha kiunoni hutofautiana na umri wa mtumiaji. Kwa kawaida, wasichana wasiovunja ungo na walioolewa wenye watoto huvaa vitambaa vyenye tarizi rahisi, inayoonyesha kuwa "maua haya hayajachanua" au "yamepukutika". Wakati msichana anapovunja ungo huanza kujipamba; anadhihirisha kukomaa kwake na matarajio yake kwenye kitambaa cha kiunoni. Kitambaa hicho kinaonyesha kuwa ameshavunja ungo, na anaruhusiwa kuchumbiwa. Wasichana wenye umri huo huenda kwenye misitu minene na kuimba nyimbo za mapenzi za kuvutia au kupiga muziki wa kuburudisha kwa majani ya miti. Vitambaa vya kiunoni wanavyovaa wasichana hawa hutariziwa kwa maua mbalimbali au wanyama wadogo kama vile peony, haibiskas, kuku, phoenix, na kipepeo. 

     Michoro kwenye vitambaa vya kiunoni hutariziwa kwa mtindo wa kukuza mambo. Michoro hiyo huonyesha matarajio ya maisha na mapenzi ya akina mama wa kabila la Wabai.

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-27