Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-28 17:59:27    
Kampuni ya teknolojia ya juu ya China barani Afrika

cri

    Hua Wei ni kampuni maarufu ya teknolojia ya juu nchini China. Katika miaka ya karibuni, kufuatana na sera za serikali ya China za kuyahimiza makampuni ya China kuanzisha shughuli zake nchi za nje, Kampuni ya Huawei imezingatia masoko ya nje. Mpaka sasa, kampuni hiyo imeanzisha ofisi zake kwenye nchi zaidi ya 20 barani Afrika.

    Bw. Mei Xiaoping ni meneja mkuu wa tawi la kampuni ya Hua Wei Afrika ya Mashariki. Alieleza kuwa, Huawei ni kampuni ya teknolojia ya juu inayoshughulikia hasa teknolojia ya upashanaji habari. Mwaka 2004, mapato ya kampuni hiyo kwenye nchi za nje yanazidi dola za kimarekani bilioni mbili. Tangu kampuni hiyo ianzishe shughuli zake barani Afrika mwishoni mwa karne iliyopita, imeanzisha ofisi yake kwenye nchi zaidi ya 20 barani Afrika. Mwanzoni mwa mwaka 2005, kutokana na shughuli zake barani Afrika, Kampuni ya Hua Wei ilianzisha matawi matatu, yakiwemo tawi la Afrika ya Mashariki nchini Kenya, tawi la Afrika ya Magharibi nchini Nigeria na tawi la Kusini mwa Afrika nchini Afrika ya Kusini. Bw Mei anasema:

    "Shughuli za Huwei zilipata maendeleo ya kasi kwenye sehemu ya kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika mwaka jana, na mapato yake mwaka 2004 yalifikia dola za kimarekani milioni 480. Mwaka huu, lengo letu ni kuzidi dola za kimarekani bilioni moja. Tawi la Afrika ya Mashariki ambalo makao yake makuu yako huko Nairobi, Kenya, linashughulikia mambo yake katika nchi jirani zikiwemo Ethiopia, Burundi, Uganda, Somalia, Rwanda na Sudan. Hivi sasa, tawi hilo lina wafanyakazi 24 kutoka China, na 26 wa Kenya, na idadi hiyo itafika zaidi ya mia moja mwishoni mwa mwaka huu."

    Bw. Mei alisema kuwa, Kenya ni makao makuu ya tawi la Afrika ya Mashariki la Kampuni ya Hua Wei. Tangu kampuni hiyo ianzishe shughuli zake nchini Kenya mwaka 1999, imeridhisha wateja kutokana na bidhaa zake bora na huduma nzuri. Mwezi Novemba mwaka 2004, kampuni kubwa zaidi ya upashanaji habari wa simu za mikononi nchini Kenya Safaricom ilisaini mkataba wa mradi wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 34 na kampuni ya Huawei.

    Naibu meneja mkuu wa tawi la Hua Wei Afrika ya Mashariki Bw. Zhou anasema,

    "Safari hii kampuni yetu imedai bei ya juu katika mkataba huo, na inamaanisha kuwa mafanikio hayo yanatokana na ubora wa bidhaa na huduma zetu, na uwezo na sifa za kampuni ya Huawei."

    Bw. Zhou alisema kuwa, ushirikiano huo unathibitisha wa ushirikiano wa muda mrefu kati ya kampuni ya Hua Wei na Safaricom ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya mawasiliano nchini Kenya, pia unamaanisha kuwa, zana za kampuni ya Hua Wei kuingia katika Kampuni ya Vodafone kwa kiasi kikubwa. Vodafone ni moja kati ya kampuni kubwa zaidi za mawasiliano duniani, ambayo inazingatia sana ubora na uwezo wa kampuni zinazotoa huduma. Katika mradi huo mkubwa, kampuni ya Hua Wei ilishinda washindani wake yakiwemo makampuni mengi maarufu ya nchi za magharibi. Katika sherehe ya kutiwa saini kwa mkataba huo, mkuu wa Kampuni ya Safaricom Bw. Mike Joseph alisema kuwa ana imani kubwa na uwezo wa Hua Wei, hii ndiyo ni sababu yake ya kuchagua kampuni hiyo kuwa mwenzi wake wa muda mrefu.

    Wakati huo huo, Kampuni ya Huawei ilisaini mikataba na Kampuni ya taifa ya Upashanaji Habari wa Simu ya Zimbabwe TELONE na Kampuni ya taifa ya Upashanaji Habari wa Simu za Mikononi wa nchi hiyo NETONE.

    Katika mradi wa ushirikiano na Kampuni ya TELONE, kampuni ya Hua Wei itatoa huduma mbalimbali kuhusu mawasiliano ya simu, ikiwemo mitambo ya ubadilishaji(exchange, switchboard), kebo ya taifa ya upelekaji, teknolojia ya CDMA na Intelligent Net IN, na mtandao mkuu wa data, na kufanya watu laki 5 kuweza kutumia simu, hatua ambayo itaboresha kwa kiasi kikubwa hali ya wasiwasi ya hivi sasa ya mawasiliano ya simu nchini humo, vilevile itatatua masuala ya mawasiliano kwenye sehemu kubwa ya vitongoji na vijiji, na kuisaidia Zimbabwe kuanzisha mtandao wa kisasa wa mawasiliano ya simu.

    Bw. Zhou alisema kwa fahari kubwa kwamba, mafaniko ya Kampuni ya Hua Wei katika Bara la Afrika si fahari ya kampuni hiyo tu, bali pia yameongeza sifa za bidhaa za kichina Kwenye bara hilo. Anasema,

    "Kampuni ya Hua Wei imefanikiwa kuingia kwenye masoko ya teknolojia ya juu barani Afrika, hali ambayo pia imeinua sifa ya bidhaa za kichina kwenye bara hilo. Zamani, bidhaa ndogo zenye bei rahisi zilizotengenezwa nchini China zilipelekwa zaidi barani Afrika, lakini sasa Kampuni ya Hua Wei imepiga hatua ya kwanza ya China kuingia kwenye soko la bidhaa za hali ya juu barani Afrika."

   

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-28