Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-31 14:57:20    
Kwenda mtaa wa Liulichang kutafuta utamaduni wa kale wa China

cri

Mzee Meng Debao mwenye umri wa miaka 57 mwaka huu ni mfanyakazi wa kuendesha gari la magurudumu matatu na amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 10. Kila siku anapita kwenye Mtaa wa Liulichang, anasema:

Mtaa wa Liulichang umekuwepo tangu enzi ya Qing ya China ya kale. Mwanzoni kwenye mtaa huo kulikuwa na matanuri mengi ya kuchoma vigae vya Liuli yaani vigae vya fahari kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kifalme.

Kama alivyosema Mzee Meng, mapema kuanzia Enzi ya Yuan ya China ya kale wakati wa karne ya 13, mamlaka ya utawala wa kifalme ilianzisha kiwanda cha matanuri ya kuchoma vigae vya Liuli. Wakati wa Enzi wa Ming kiwanda hicho kilipanuliwa zaidi. Ilipofika karne ya 17, kutokana na upanuzi wa mji wa Beijing, kiwanda hicho kilihamia nje ya mji, lakini jina lake Liulichang limedumishwa kwenye mtaa huo.

Wakati wa Enzi ya Qing ya karne ya 17, maofisa wengi wa serikali waliishi kwenye sehemu iliyo karibu na Kiwanda cha kutengeneza vigae vya fahari Liuli, kwani sehemu hiyo ni karibu sana na karsi la kifalme, na wanafunzi wengi kutoka mikoa mingine nchini waliokuja Beijing kupitia mtihani pia walivutiwa na sehemu hiyo. Ili kutosheleza mahitaji ya maofisa na wanafunzi, wafanyabiashara wa vitabu walianzisha mabanda yao au kujenga maduka ya kuuzia vitabu, hivyo mtaa wa Liulichang ukaendelea kuwa soko kubwa kabisa la vitabu la Beijing, na vitu vyote vinavyohusika na vitabu pia viliuzwa kwenye maduka ya huko.

Mtaa wa Liulichang wa hivi leo umepanuliwa baada ya kufanyiwa ukarabati na serikali ya China mwanzoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita. Mtaa huo unagawanyika kuwa mtaa wa mashariki na wa magharibi, nyumba za kando ya njia zilijengwa kwa matofali ya aina ya kale, mapambo ndani ya nyumba yakiwemo pamoja na michongo ya matofali au mbao pamoja na michoro ya mafuta ya rangi, ambayo yameonesha mtindo wa jadi wa sehemu ya wakazi wa Beijing katika kipindi cha mwisho cha Enzi ya Qing.

Hivi leo kwenye mtaa huo kuna maduka zaidi ya 100. Maduka yaliyoko kwenye mtaa wa mashariki yanauza mawe ya marumaru, kauri, jade na vyombo vya mbao. Na maduka yaliyoko kwenye mtaa wa magharibi yanauza hasa maandiko na michoro pamoja na vitu vya kale. Hata vitu vyote vya kila kipindi cha historia ya China vinaweza kupatikana katika maduka hayo, kama vile vitu halisi vya kale vyenye thamani kubwa, pia kuna vitu vilivyotengenezwa kwa kuiga vitu halisi vya kale, na wauza duka wanaweza kuandika wazi bei za vitu na kuwaambia wateja vipi ni vitu halisi na vipi ni vya bandia.

Miongoni mwa maduka hayo, kuna maduka kadha wa kadha yenye historia ya zaidi ya miaka mia moja. Duka la Qingmi linaloendeshwa na Bwana Jia Zhiren ndiyo duka lenye historia zaidi ya miaka 300. Bwana Jia alisema:

Duka la Qingmi ni duka la kuhifadhi vitabu, lilikuwa duka maarufu wakati wa Enzi ya Qing, ambapo maofisa wengi wa kasri la kifalme walitembea duka hilo kila mara.

Mtaa wa Liuli unawavutia watu wa sehemu mbalimbali duniani, Bibi Madeleine Foqde kutoka Sweden alisema:

Napenda sana mtaa huo wenye utulivu na usalama ambao ni alama ya utamaduni wa kale wa China. Kila ukitembea maduka ya mtaa huo unaweza kuona vitu vingi vya kale vya China.

Idhaa ya kiswahili 2005-01-31