Uchaguzi mkuu wa Iraq ulifanyika tarehe 30 kwa mpango uliopangwa chini ya kiwingu cha mashambulio ya mabomu yaliyofanywa na wenye silaha mara kumi kadhaa.
Wachambuzi wanaona kuwa huu ni uchaguzi usio wa kawaida kabisa ambao unafaa kuandikwa katika kitabu cha rekodi za Guinness, kwa sababu hadi siku ilipofanyika uchaguzi huo hali kama idadi gani ya vituo vya kupigia kura viliwekwa, wapiga kura wenye haki ni wangapi, matokeo ya uchunguzi wa maoni ya wananchi kuhusu uchaguzi huo yalikuwaje na matokeo ya uchaguzi huo yatatangazwa siku gani, yote hayajatangazwa. Uchaguzi unaofanyika katika mazingira kama hayo matokeo yake yatakuwa halali au yataheshimika? Yanatiwa wasiwasi.
Kwanza, uchaguzi huo unafanywa kwa kuendeshwa na nchi za nje. Vikundi vingi vya siasa nchini Iraq vinaona kuwa hali ya uchaguzi huo mkuu haijaiva, lakini Marekani inashikilia ufanywe kama ulivyopangwa kwa ajili ya maslahi yake. Rais Bush wa Marekani aliwahi kusema kuwa huu ni "uchaguzi mtukufu" katika historia ya Iraq, Marekani inataka kuisaidia Iraq kupata demokrasia, na inawahamasisha watu wa Iraq wawe "washupavu" wa kupiga kura bila kuogopa tishio la ugaidi na waioneshe dunia kuwa "magaidi hawawezi kuzuia demokrasia ya Iraq".
Pili, uchaguzi huo unafanyika katika hali mbaya ya usalama nchini Iraq. Kabla ya uchaguzi huo, watu wenye siasa kali walitangaza kuwa watafanya mashambulio dhidi ya uchaguzi huo, na milipuko ya mabomu ilitokea mfululizo. Ingawa serikali ya muda ya Iraq na muungano wa jeshi la Marekani na Uingereza vilichukua hatua nyingi za kuimarisha usalama, lakini hazikufua dafu. Matukio ya milipuko yalipoza sana joto la upigaji kura, na hali ya kutotokea hata mpiga kura mmoja katika vituo vingi katika siku ya kupiga kura ilitokea.
Tatu, lengo la kufanya uchaguzi mkuu ni kupata serikali halali na kumaliza hali ya Iraq kukaliwa na nchi za nje, hili ni tumaini la pamoja la vikundi vyote vya siasa nchini Iraq, lakini wakati gani ni mwafaka kwa kufanya uchaguzi huo ndio tatizo la vikundi hivyo kuhitilafiana. Waislamu wa madhehebu ya Shiya wana tamaa ya kupata nguvu kubwa ya madaraka kutokana na hali yao ya kuwa na idadi kubwa ya asilimia 60 ya Wairaq, kwa hiyo wanaunga mkono uchaguzi huo ufanyike kwa mpango uliopangwa, na watu wa Kurd pia wanatamani kuufanya uchaguzi huo bila kuchelewa ili wapate bunge lao na kupata nafasi katika serikali kuu. Lakini kwa upande mwingine Waislamu wa madhehebu ya Suni wanaochukua asilimia 30 ya watu wa Iraq hawana hamu na uchaguzi huo.
Nne, nguvu za ukaguzi wa uchaguzi huo hazitoshi, hasa wachunguzi kutoka nchi za nje. Kutokana na takwimu zilizotangazwa na idara husika za Iraq, wakaguzi elfu 18 wanatoka kutoka idara za ukaguzi, na elfu 22 wanatoka kutoka vikundi vinavyoshiriki katika uchaguzi huo, lakini kutokana na marufuku ya kutembea, wakaguzi hao hawakuweza kufika kwenye nafasi zao za kazi katika siku ya uchaguzi. Kutokana na takwimu, idadi ya wakaguzi ni karibu sawa na idadi ya wakaguzi katika uchaguzi wa Palestina, lakini wapiga kura nchini Iraq ni mara kumi kuliko wapiga kura wa Palestina, na kutokana na hali mbaya ya usalama wakaguzi kutoka nchi za nje wako 120 tu ambao ni idadi ndogo sana ikilinganishwa na idadi ya wakaguzi wa ng'ambo waliokuwa karibu elfu moja nchini Palestina. Msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Iraq hivi karibuni amesema kuwa kazi ya Umoja wa Mataifa nchini Iraq ni kutoa misaada ya kiufundi na ushauri tu na hautashiriki kwenye ukaguzi wa uchaguzi huo, wala hautatoa maoni yoyote kuhusu matokeo ya uchaguzi huo. Kwa hiyo watu wengi wanatia wasiwasi kuhusu uhalali ya uchaguzi huo.
Wachambuzi wanaona kuwa kutokana na mazingira kama hayo yasiyo ya kawaida, uchaguzi huo hautaweza kugeuza hali mbaya ya usalama. Hata hivyo serikali mpya itakayochaguliwa ni tofauti kabisa na ya muda, hakika itaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.
Idhaa ya kiswahili 2005-01-31
|