Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-31 20:31:10    
Maendeleo ya Afrika yakabiliwa na fursa na changamoto kubwa

cri

    Mkutano wa nne siku mbili wa viongozi wa serikali wa nchi za Umoja wa Afrika ulifunguliwa leo huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria. Viongozi wa nchi na wawakilishi wa ngazi ya juu wa serikali za nchi wanachama 53 wa Umoja wa Afrika wanafanya majadiliano kuhusu masuala mengi yakiwemo ya migogoro ya kikanda, usalama wa chakula, tiba, mambo ya afya pamoja na mageuzi ya Umoja wa Mataifa. Vyombo vya habari vinaona kuwa nchi za Afrika zinakabiliwa na fursa nzuri ya maendeleo, wakati huo huo zinakabiliwa changamoto kubwa za aina mbalimbali.

    Katika miaka michache iliyopita, migogoro mingi iliyo kuweko kwa muda mrefu na kukwamisha maendeleo ya Afrika na, imeanza kupungua, hali ambayo inafanya hali ya sehemu hiyo kuelekea kutulia: serikali ya Sudan imeafikiana na jeshi linaloipinga serikali lililoko kusini mwa nchi hiyo kusimamisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu zaidi barani Afrika; vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi za Liberia, Sierra Leone na nchi nyingine vimemalizika, na ujenzi mpya wa nchi hizo umeanza; makundi mbalimbali yaliyokuwa yakipambana nchini Somalia yameafikiana kwenye mkataba na kuchagua bunge jipya na rais wa mpito wa nchi hiyo.

    Hali ya amani na utulivu iliyotokea katika miaka ya karibuni katika baadhi ya nchi za Afrika imetoa fursa kwa maendeleo ya uchumi wa sehemu hiyo. Katika muda wa karibu miaka kumi iliyopita, ingawa uchumi wa dunia haukuweza kupata ongezeko la utulivu, lakini uchumi wa Afrika ulikuwa na ongezeko kwa taratibu. Nchi nyingi za Afrika katika miaka mingi iliyopita zilitekeleza sera mwafaka za uchumi, kushikilia kurekebisha miundo wa uchumi na ziliboresha hali ya uchumi. Kutokana na taarifa iliyotolewa na kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa, ongezeko la uchumi wa Afrika katika mwaka 2003 lilikuwa 3.6% na mwaka huu linaweza kufikia 4.4%. Mbali na hayo, kufufuka hatua kwa hatua kwa uchumi wa dunia katika miaka ya karibuni pia kumehimiza ongezeko la uchumi wa Afrika, hususan kuongezeka kwa mahitaji ya mali-ghafi za Afrika na kupanda kwa bei zake katika masoko ya kimataifa.

    Wachambuzi wanaona kuwa kubadilika kwa hali ya usalama ya Afrika na kuwa nzuri na maongezeko ya mfululizo ya uchumi wa Afrika vimeleta fursa nzuri sana kwa maendeleo ya Afrika, lakini hata hivyo, njia ya nchi za Afrika ya kutafuta amani na maendeleo kamwe haitakuwa fupi na nyepesi.

    Kwa upande mmoja, ingawa baadhi ya migogoro ya Afrika imetatuliwa, lakini amani katika sehemu nyingi bado ni dhaifu sana, tena baadhi ya migogoro mipya imeshatokea na kuleta athari mbaya kwa utulivu wa sehemu hiyo. Ujenzi mpya wa Liberia baada ya vita kumalizika unakabiliwa na matatizo mengi; migogoro ya Darfur nchini Sudan na Cote d'ivoire imekuwa mbaya siku hadi siku; na hali ya sehemu ya mashariki ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imefikia hatua ya kutoweza kudhibitiwa.

    Kwa upande mwingine, ingawa uchumi wa Afrika umekuwa na ongezeko, lakini karibu nusu ya idadi ya watu walioko kwenye sehemu ya kusini mwa Sahara bado wanaishi chini ya kiwango cha umaskini, nchi nyingi za Afrika bado ziko mbali na "Lengo la maendeleo ya milenia mpya" la Umoja wa Mataifa la kupunguza nusu ya idadi ya watu maskini itakapofika mwaka 2015. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan katika sherehe ya ufunguzi wa mkutano uliofanyika siku ile ile, alisema kuwa Afrika imekuwa nyuma kuliko baadhi ya sehemu za duniani katika utekelezaji wa "lengo la maendeleo ya milenia mpya", baadhi ya nchi hizo bado ziko mbali sana na lengo la kutokomeza hali ya umaskini na maradhi. Licha ya hayo, magonjwa na mzigo mkubwa madeni ya nchi za Afrika pamoja na hali mbaya ya umaskini pia vimekwamisha vibaya maendeleo ya sehemu hiyo.

    Umoja wa Afrika ukiwa jumuiya ya kiserikali yenye nguvu kubwa zaidi miongoni mwa nchi za Afrika, hadhi yake imekuwa muhimu siku hadi siku. Hali hiyo imeonesha kuwa nchi za Afrika zimekuwa na maoni ya namna moja katika kutatua migogoro, kuhifadhi amani na usalama wa sehemu hiyo na kuhimiza maendeleo ya uchumi kwa nguvu zao za pamoja. Lakini masuala ya upungufu wa fedha na uzoefu yamekuwa makubwa na kupunguza ufanisi wa juhudi za Umoja wa Afrika.

    Kwa ujumla, njia ya Afrika ya kuondokana kabisa na migogoro ya vita na hali ya umaskini itakuwa mbali na yenye shida nyingi, inahitaji nchi za Afrika zijitahidi zaidi na kuhitaji misaada ya jumuiya ya kimataifa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-31