Mkutano wa 5 wa mwaka wa Baraza la Jumuiya ya Kimataifa, ambao ulifanyika kwa siku 5, ulifungwa tarehe 31 mwezi Januari katika mji wa Porto Alegre nchini Brazil. Ikilinganishwa na mikutano ya miaka iliyopita, mkutano wa mwaka huu umezingatia zaidi masuala la kijamii yakiwa ni pamoja na kuondoa umaskini, utamaduni wa aina mbalimbali, elimu kwa watu wote, hifadhi ya maslahi ya wanyonge, mtindo mpya wa maendeleo ya jamii na uchumi pamoja na haki za binadamu, ambapo mapendekezo mengi husika yametolewa.
Mkutano wa mwaka huu ni mkutano mkubwa kabisa tangu kufanyika kwa mkutano wa baraza hilo, idadi ya washiriki ilizidi laki 1.5 wakiwemo rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil, rais Hugo Chavez Farias wa Venezuela pamoja na watu wengi mashuhuri duniani. Mada zilizojadiliwa katika mkutano huo ni nyingi zaidi kuliko mikutano ya miaka iliyopita, ambazo zimezidi 11. Katika siku chache zilizopita washiriki walihudhuria mikutano, mijadala na shughuli za aina mbalimbali zaidi ya 2,500 kwa jumla na kutoa mapendekezo zaidi ya 350.
Suala la umaskini liliendelea kuwa ni mada muhimu katika mkutano wa mwaka huu. Ili kuanzisha harakati za kukomesha hali ya umaskini duniani, "mkutano wa vitendo vya kukomesha hali ya umaskini duniani" ulifanyika katika siku ya pili baada ya mkutano wa mwaka kufunguliwa. Rais Lula wa Brazil alihudhuria mkutano huo na kutoa hotuba, akisema kuwa suala la umaskini ni moja ya suala kubwa kabisa linalowakabili binadamu. Alitoa wito wa kutaka nchi maskini ziungane, kuimarisha ushirikiano wao na ushirikiano kati yao na nchi nyingine duniani ili kutokomeza umaskini. Licha ya hayo, rais Lula aliukosoa msimamo wa kutojitahidi wa viongozi wa baadhi ya nchi zilizoendelea. Alisema kuwa atawasilisha tena suala hilo kwenye mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwezi Septemba mwaka huu ili kuwasihi viongozi wa nchi mbalimbali duniani washiriki pamoja kutatua suala hilo.
Suala la kuweko kwa mitindo ya aina mbalimbali halikuzingatiwa kama na mkutano wa mwaka huo. Katika muda wa mkutano wa baraza wa mwaka huu, zilioneshwa ngoma, michezo ya kuigiza, nyimbo na muziki, maonesho ya picha na vitu vya sanaa za kazi za mikono zaidi ya 500. Washiriki wa mkutano wanaona kuwa ni utamaduni wa makabila mbalimbali, ambao umeunda dunia yetu yenye mambo na vitu mbalimbali vya kupendeza. Hivyo, mataifa yote duniani yanapaswa kuishi pamoja kwa masikilizano na kufundishana. Dunia isiwe na sura au utamaduni wa aina moja tu, wala haifai kupachika utamaduni au mtazamo wa taifa fulani kwa mataifa mengine, njia ambayo haitakubaliwa na watu wengine wala haifai kwa maendeleo ya ustaarabu wa binadamu.
Mkutano mkuu wa mwaka huu pia ulifanya mijadala mingi. Washiriki wa mijadala wamesema kuwa, elimu inatakiwa kuwekwa katika eneo la haki za binadamu. Tabia ya binadamu ni kuboresha kwa mfululizo hali yake, kujifunza elimu za aina mbalimbali, hivyo washiriki wameona kuwa katika jamii yenye elimu na ustaarabu, kukataa haki za elimu za watu ni kukiuka haki za binadamu za kupata haki za elimu zilizovumbuliwa na binadamu.
Mkutano mkuu wa mwaka huu pia ulialika watu wengi mashuhuri duniani kushiriki kwenye mijadala kuhusu masuala mengi likiwemo la demokrasia. Watu wengi wamekosoa hali ya demokrasia iliyopo hivi sasa. Mwandishi wa vitabu wa Ureno Bw. Sallamaco aliona kuwa jambo muhimu la kujenga utaratibu mpya wa kisiasa, kiuchumi na kijamii ni kubadilisha imani ya watu.
Kupinga vita na kuhifadhi amani ni mambo yaliyofuatiliwa zaidi na watu katika mkutano mkuu wa baraza wa mwaka huu. Washiriki walifanya maandamano mara nyingi wakitaka kupinga vita na vitendo vya matumizi ya nguvu. Katika siku ya kufungwa kwa mkutano mkuu wa mwaka huu, washiriki na watu wanaopinga vita kutoka sehemu mbalimbali za dunia, walikwenda kwenye mitaa ya mji wa Porto Alegre wakitaka Marekani na Israeli ziondoke mara moja kutoka Iraq na Palestina, na walichoma moto picha ya rais Bush wa Marekani.
Idhaa ya Kiswahili 2005-02-01
|