Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-02 16:10:07    
Tajiri kijana wa China Ding Lei

cri

Tarehe 10 mwezi Januari mwaka 2005, Bw. Ding Lei alichangia dola za kimarekani milioni 1.2 kwa chama cha msalaba mwenkundu cha China ili kuwasaidia watu waliokumbwa na maafa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi kwenye bahari ya Hindi. Habari ilisema kuwa, sasa Bw. Ding lei ni mtu aliyechangia pesa kubwa nchini China.

Bw. Ding Lei mwenye umri wa miaka 34, mwaka 2003 alichukua nafasi ya kwanza miongoni mwa matajiri wa China, ambapo alikuwa na mitaji Yuan bilioni 7.5 ambayo ni karibu ya dola za kimarekani milioni 100.

Mwezi Okatuba mwaka 1971 Ding lei alizaliwa huko Ningbo, mkoani Zhenjiang, mashariki mwa China. Mwaka 1993 alihitibu kutoka chuo kikuu cha sayansi na teknolojia ya elekchoniki cha Chengdu. Mwaka 1993-1995 alikuwa mhandisi wa Idara ya mawasiliano na simu ya mji wa Ningbo; mwaka 1995-1996 alifanya kazi katika Kampuni ya Sybase huko Guangzhou, Kusini mwa China; mwezi Juni mwaka 1997 alianzisha kampuni ya Netease, mwaka huu alianzisha mfumo wa barua pepe (Email) wa lugha mbili; mwaka 1997-1999 Kampuni ya Netease ilishughulikia utafiti wa software na mtandao wa internet; mwezi Juni mwaka 2000, Kampuni ya Netease iliingia kwenye soko la hisa la NASDAQ?

Mapato yake makubwa katika chuo kikuu ni kufikiri kwa chini juu

Bw. Ding lei alisema kuwa, katika masomo yake ya miaka mine ya chuo kikuu alijifunza uwezo wa kujifikiri. Kuanzia muhula wa pili alijifunza mwenyewe bila kuingia darasani. Baada ya juhudi zake kubwa alipata ujuzi vilevile.

Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu alianza kushughulikia mambo ya mtandao wa internet, alipopata ujuzi wa internet alitambua kuwa, mtandao wa internet utaleta mabadiliko makubwa kwa maisha ya watu.

Hatua ya kwanza ya maisha yake-kukubaliana na changamoto

mwaka 1995 aliacha kazi yake kwenye idara ya mawasiliano na simu ya mji wa Ningbo. Ingawa azimio yake ilipingwa na familia zake lakini alikuwa ameamua kwenda nje na kuanza kutafuta ajira mpya.

Mwezi Mei mwaka 1995 alikwenda Guangzhou na kufanya kazi katika kampuni ya Sebyse. Mwanzoni maisha ni magumu, rafiki yake alisema kuwa, hivi sasa Ding lei anapenda kupika chakula na kucheza muziki, sababu muhimu ni kwamaba, wakati ule vitu hivi viwili vilikuwa ni mambo yaliyomfurahisha tu. Mbali na hayo, maisha yake ni kufanya kazi kwa bidii tu.

Baada ya kufanya kazi katika kampuni ya Sebyse ya Guangzhou, Ding Lei alikuwa na mawazo ya kuanzisha kampuni ya mtandao wa internet pamoja na watu wengine. Kuhusu hali hiyo, alisema kuwa, kuondoka kampuni ya Sybase pia ni ngumu, kwa sababu kampuni aliyoikwenda ni ndogo sana, lakini alikuwa na imani kwamba, kampuni hiyo italeta athari kubwa kwa mambo ya mtandao wa internet ya China. Baada ya mwaka mmoja, alikuwa na uzoefu wa kutosha katika teknolojia na ufundi wa internet. Mwezi Mei mwaka 1997 aliamua kuanzisha Kampuni ya mtandao wa internet-Netease, alikuwa na imani atafanikiwa kutoka shughuli zake.

Idhaa ya kiswahili 2005-02-02