Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-02 20:06:40    
Chombo cha kwanza cha uchunguzi kilichotua kwenye sayari ya Titan ya Saturn

cri

    Chombo cha uchunguzi kijulikanacho kwa jina la "Huygens" ambacho kilirushwa kutoka kwenye dunia zaidi ya miaka 7 iliyopita, kilitua kwenye Titan, sayari iliyo kubwa kabisa ya Saturn.

    Sayari ya Titan iligunduliwa na mnajimu wa Uholanzi Bw. Christian Huygens mwaka 1655 kwa darubini aliyoitengeneza yeye mwenyewe. Baada ya kufanya uchunguzi mnajimu huyo alikisia kuwa mazingira ya Titan yanafanana na ya dunia ya awali. Uchunguzi unaofanywa kuhusu Titan utamsaidia binadamu kufahamu siri ya uhai. Hivyo, idara ya safari za anga ya juu ya Ulaya ilisanifu mahsusi chombo cha uchuguzi kwenye Titan, ili kuadhimisha ugunduzi mkubwa wa Bw. Christian Huygens, na waliamua chombo hicho cha uchunguzi kitumie jina la mnajimu huyo.

    Chombo cha "Huygens" kina uzito wa kilo 319, umbo lake ni kama kombe ya baharini, ambayo sehemu yake ya mbele kuna kitu mfano wa ngao ya kuzuia joto, chombo hicho kina miamvuli miwili ya kusaidia kutua kwa usalama. Chombo hicho kina vifaa 6 vya kupima nguvu ya mkandamizo wa hewa, joto, kasi ya upepo na vitu vilivyoko katika hewa ya huko, na vitatoa data nyingi kwa wanasayansi katika uchambuzi kuhusu sayari ya Titan.

     Wakati chombo hicho kikiwa kwenye umbali wa kilomita 1,200 kutoka kwenye sayari ya Titan, mtambo ulioko katika chombo cha "Huygens" ulifyatuka na kuelekea kwenye Titan kwa kasi ya kilomita elfu 22 kwa saa, ambapo kitu kilichofanana na ngao kilichowekwa kwenye sehemu ya mbele ya chombo hicho kinafanya kazi ya kuzuia joto ili kuepusha chombo hicho kisilipuke kutokana na mwendo mkali. Wakati chombo hicho kilipofikia umbali wa kilomita 190 kutoka Titan, chombo hicho kilitengana na ngao ya kuzuia ujoto. Chombo kilipofikia umbali wa kilomita 170, kasi yake ilipungua hadi kilomita 1,400 kwa saa. Baada ya hapo chombo cha "Huygens" kilifungua miamvuli yake mitatu, na kilipofikia umbali wa mita mamia kadhaa, kiliwasha taa zake kubwa ili kuangaza vitu vilivyoko kwenye sehemu ya juu ya Titan.

    Kabla ya hapo, chombo cha uchunguzi cha "Huygens", kilikuwa kimelala usingizi kwa miaka 7 kwenye chombo cha Marekani kilichokuwa kikikibeba kijulikanacho kwa jina la "Cassini". Tarehe 25 mwezi Desemba mwaka jana, chombo cha "Huygens" kiliachana na chombo cha "Cassini" na kuelekea kwenye Titan ili kutekeleza majukumu yake. Katika muda huo wote, chombo cha "Huygens" kilikuwa kimelala usingizi, na zana zote zilizoko ndani ya chombo hicho hazikufanya kazi hadi zilipozinduliwa saa chache tu kabla ya kufika kwenye Titan.

    Muda wa kutua kwa chombo cha "Huygens" ni kama muda wa kujiua, ambao chombo kinapeleka data kilizopata kwa chombo kilichokibeba cha "Cassini" hadi betri yake ilipoishiwa nguvu baada ya nusu saa.

Picha husika>>


1  2  3  4