Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-02 20:53:40    
Wataalamu wa China wazungumzia mfumo wa kutoa tahadhari kabla ya maafa ya tsunami

cri

    Kwa kuwa kutoweza kutoa tahadhari kuhusu maafa, maafa makubwa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi kwenye Bahari ya Hindi mwishoni mwa mwaka 2004 yalisababisha vifo vya watu laki 1.7. Maafa hayo yameonya kila nchi iliyo karibu na bahari yapaswa kutambua umuhimu wa kuanzishwa kwa mfumo wa kutoa tahadhari kuhudu maafa.

    Ili kufahamu vizuri zaidi mfumo wa kutoa tahadhari kabla ya maafa yanayosababishwa na tetemeko la ardhi kwenye bahari, kwanza tunahitaji kujua sababu tatu za maafa hayo. Sababu ya kwanza ni tetemeko la ardhi, ya pili ni mlipuko wa volkano, na ya tatu ni maporomoko ya ardhi . Asilimia 95 ya maafa yanasababishwa na tetemeko la ardhi kwenye bahari, maafa hayo huleta uharibifu mkubwa kabisa, mwishoni mwa mwaka jana maafa yaliyotokea kwenye bahari ya Hindi ndiyo yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi kwenye bahari.

    Mjiolojia maarufu wa China, ambaye pia ni mtafiti katika taasisi ya sayansi ya China Bw. Chenyu alifahamisha masharti matatu yanayoweza kuleta maafa yanayosababishwa na tetemeko la ardhi kwenye bahari, akisema:

    "Kuna masharti matatu yanayoweza kuleta maafa yanayosababishwa na tetemeko la ardhi kwenye bahari, likikosekana moja kati ya hayo, maafa hayo hayawezekani kutokea. La kwanza ni kuwa tetemeko la ardhi hakika linaweza kutokea kwenye bahari yenye kina kirefu zaidi ya kilomita 1 kutoka uso wa bahari, la pili ni kuwa ni tetemeko kubwa la ngazi ya 7 linalotokea chini ya bahari ambalo linaweza kusababisha maafa kwenye bahari, la tatu ni kuwa tetemeko la ardhi linalotokea chini ya bahari likiyafanya maji ya bahari kupanda juu litasababisha dhoruba au mawimbi makubwa kwenye bahari."

    Lakini matetemeko mengi ya ardhi yanayotokea chini ya bahari hayawezekani kusababisha maafa kama hayo.

    Wataalam wamefahamisha kuwa kutokana na sababu na hali maalum zinazoleta maafa yanayosababishwa na tetemeko la atdhi kwenye bahari, mfumo wa kutoa tahadharai kabla ya maafa kutokea unapaswa kulingana na vigezo vitatu, yaani mfumo huo unaweza kugundua kwa wakati tetemeko la ardhi kutokea chini ya bahari na mabadiliko ya usawa wa bahari; kuweza kuthibitisha tetemeko la ardhi litasababisha maafa kwenye bahari au la kutokana na uchambuzi kuhusu tarakimu zilizopatikana katika uchunguzi na kuweza kukadiria nguvu ya maafa, maeneo ya sehemu zitakazoathiriwa na muda itakayochukua kufika pwani ya nchi; na kuweza kutoa tahadhari kwa wakati kwa sehemu zitakazokumbwa na maafa, na kutekeleza mpango uliowekwa kwa ajili ya kukabiliana na maafa.

    China imeanza kuimarisha uwezo wa kutoa tahadhari kabla ya kutokea kwa maafa yanayosababishwa na tetemeko la ardhi kwenye bahari kwa kufuata vigezo hivyo vitatu kuanzia miaka 70 ya karne iliyopita, na imejenga mfumo wa aina hiyo hatua kwa hatua. Kituo cha utabiri wa mazingira ya bahari cha China kinashughulikia utafiti wa mfumo huo, mtafiti wa kituo hicho Bw. Yu Fujiang amefahamisha kuwa mfumo wa China wa kutoa tahadhari kabla ya maafa kutokea una sehemu mbili, akisema:

    "Sehemu ya kwanza ni mfumo wa ufuatiliaji na uchunguzi. Mfumo huo unapata tarakimu kutoka vituo vya usimamizi vilivyoko kwenye sehemu ya pwani na visiwani, idara ya tetemeko la ardhi ya China na hahari ya Pasifiki ya kutoa tahadhari kabla ya maafa kutokea. Ya pili ni mfumo wa kutoa tahadhari. Tutatoa tahadhari baada ya kuzichambua tarakimu, kama vile, maafa yakitokea kwenye sehemu fulani ya bahari ya Pasifiki, tunaweza kufanya hesabu na kufahamu muda ambao maafa hayo yatakayochukua kufika China."

    Imefahamika kuwa China imeweka vituo vya ufuatiliaji na uchunguzi zaidi ya 70 kwenye sehemu ya pwani na visiwani, na takwimu kutoka vituo hivyo vitapelekwa kwenye mfumo wa usimamizi ulioko Beijing kwa kupitia satlaiti, na wanasayansi wa huko wanaweza kusimamia mabadiliko ya usawa wa bahari ya kila wakati. Aidha, mfumo huo unaungana na vituo maarufu kabisa duniani, kama vile kituo cha bahari ya Pasifiki cha kutoa tahadhari kabla ya maafa kutokea, hivyo mfumo huo unaweza kupata takwimu zenye usahihi mkubwa kabisa wakati wowote.

    Mtafiti wa kituo cha utabiri wa mazingira ya bahari cha China Bw. Li Xuekun ambaye anashughulikia kutafiti mfumo wa kutoa tahadhari kabla ya maafa kutokea kwenye bahari, amefahamisha kuwa mara baada ya kupata habari kuhusu maafa, mfumo huo uatatoa tahadhari mwenyewe.

    Ingawa China ina uwezo wa kutoa tahadhari kabla ya kutokea maafa yanayosababishwa na tetemeko la ardhi kwenye bahari, lakini mfumo huo bado unatakiwa kuboreshwa ili utoe utabiri sahihi zaidi. Mtabiri wa ngazi ya juu wa kiuto cha utabiri wa mazingira ya bahari cha China Bi. Linlin alisema:

    "Hivi sasa China haijaweka maboya kwenye sehemu za bahari zilizoko mbali na pwani, lakini Japan na Marekani zimefanya hivyo. Aidha, tunapaswa kuweka vyombo vya usimamizi kwenye visiwa vyote, na kuinua uwezo wa mawasiliano, hasa mawasiliano kupitia satlaiti."

    Boya lililotajwa na Bi. Linlin ni chombo cha ufuatiliaji na uchunguzi kinachoweza kuelea kwenye bahari, chombo hico kinaweza kupata habari kuhusu ukubwa wa mawimbi, kasi yake na mwelekeo wake, na kupeleka habari hizo kupitia satlaiti kwenye mfumo wa kutoa tahadhari. Bi. Linlin ameona kuwa China inapaswa kuweka maboya kwenye sehemu za bahari zenye uwezekano mkubwa wa kutokea maafa.

    Wataalam wameainisha kuwa kukamilisha mfumo wa kutoa tahadhari kabla ya tsunami kutokea ni sehemu moja ya kupunguza maafa yanayosababishwa na tetemeko la ardhi kwenye bahari. Katika siku za usoni, China inapaswa kufanya mazoezi ya kukabiliana na maafa mara kwa mara kwenye sehemu za pwani, na kuwaambia wakazi wa pwani na watalii waondoke sehemu ya pwani na kwenda mahali pa juu wakati mawimbi makubwa yanapokaribia.

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-02