Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-03 21:19:10    
Lengo la ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani ni kuondoa tofauti ya maoni kati ya Marekani na Ulaya

cri

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Condoleezza Rice ambaye alichukua wadhifu huo wiki moja tu iliyopita leo ameanza kufanya ziara nchini Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Ubelgiji, Luxemburg, Polland, Uturuki, Israel na Palestina. Shughuli nyingi za kidiplomasia zilizofanywa na serikali ya Rais Bush aliyeshika tena wadhifa wa urais nusu mwezi uliopita katika nchi za Ulaya na Mashariki ya kati zimewakumbusha watu uhusiano usio mzuri uliopo kati ya Ulaya na Marekani katika miaka ya karibuni. Watu wengi wanaona kuwa, ziara ya Bi. Rice inalenga kuondoa tofauti ya maoni kati ya Marekani na Ulaya.Kwa ujumla tofauti hiyo ya maoni iko katika vita vya Iraq, mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati na Suala la nyuklia la Iran.

Vita vya Iraq viliwahi kusababisha mkwaruzano mkubwa kabisa katika miaka ya karibuni kati ya Ulaya na Marekani. Mwaka 2003, Ufaransa, Ujerumani na Russia zilipinga kithabiti Marekani kuanzisha vita nchini Iraq bila ya kupata idhini ya Umoja wa Mataifa. Mabishano kati ya pande hizo mbili kwenye Baraza la Usalama yamesababisha pengo katika uhusiano wa kiwenzi wa zamani. Baada ya vita vya Iraq, Bi. Rice ambaye alikuwa msaidizi wa mambo ya usalama wa taifa alipendekeza kwa Rais Bush "kuiadhibu Ufaransa, kuipuuza Ujerumani na kuisamehe Russia", na kusababisha uhusiano kati ya Marekani na Ulaya kuwa mbaya zaidi, hata Marekani ilipoitaka NATO ishiriki kwenye mambo mengi nchini Iraq, nchi za Ulaya hazikutoa jibu la wazi. Na Rais Bush aliposherehekea "mafanikio kabisa" katika siku kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu wa Iraq, nchi za Ulaya zilionesha furaha ya kiasi tu. Madhara yaliyolewa na vita vya Iraq kwenye uhusiano kati ya Marekani na Ulaya bado yanaonekana. Ili kutofanya mambo peke yake, na "kubandika chapa wazi ya kimataifa" kwenye vita vya Iraq, bado ni fursa kwake kuboresha uhusiano na "nchi kongwe za Ulaya" zikiwemo Ufaransa na Ujerumani wakati ambapo Rais Bush alianza kushika wadhifa wa urais kwa mara ya pili na uchaguzi mkuu ulimalizika nchini Iraq.

Kuhusu suala la Palestina na Israel, pia kuna tofauti kubwa kati ya misimamo ya nchi za Ulaya na Marekani. Ni wazi kuwa katika miaka mingi iliyopita, kitendo cha Marekani cha kuipendelea Isreal kimeleta athari mbaya kwa mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati, lakini msimamo wa nchi za Ulaya ni wa uwiano, zinapoelewa mahitaji ya usalama ya Israel, pia zimeipatia Palestina msaada na uungaji mkono mkubwa wa kimataifa. Kiongozi wa zamani wa Palestina Bw. Yasser Arafat alipofariki dunia, shughuli nyingi za kidiplomasia zilifanyika duniani, na jumuiya ya kimataifa ilitumai kuwa mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati utapata maendeleo kadhaa. Nchi za Ulaya zikitumia fursa hii, zitaifanya Marekani kusikitika sana kwani ilishiriki kwenye mambo hayo kwa miaka mingi lakini haikusifiwa hata kidogo. Hivyo siku kadhaa zilizopita, Bi. Rice alisema tena kuwa, serikali ya Rais Bush itaendelea kutoa mchango katika mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati. Kuziweka Palestina na Israel kwenye ratiba yake ya ziara ni kwa ajili ya kuonesha kuwa Marekani bado ni msuluhishi wa kwanza katika mchakato huo.

Tofauti nyingine kubwa ni katika suala la nyuklia la Iran. Msimamo wa Marekani katika suala hilo ni thabiti sana. Rais Bush aliwahi kusema kuwa, kuna uwezekano kuwa Marekani huenda itatatua suala hilo kwa hatua za kijeshi. Makamu wa rais Richard Cheney pia alitisha kuwa, Marekani imeichukua Iran kuwa ni ya kwanza kwenye orodha ya nchi zinazoanzisha vurugu. Watu wana wasiwasi kuwa Marekani itaishambulia Iran. Lakini tofauti na suala la Iraq, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zote zinashikilia kithabiti kuwa hatua ya kidiplomasia ni njia pekee ya kutatua suala la Iran, na zimefanya mazungumzo na Iran kwa muda mrefu na kupata jibu zuri kutoka Iran. Wachambuzi wanaona kuwa, Marekani kutokuwa na msimamo thabiti safari hii ni kwa sababu haikutaka kuwa na tofauti kubwa zaidi na Ulaya kama katika suala la Iraq. Hivyo katika hali hiyo ni muhimu sana kwa Rais Bush kumtuma Bi Rice kufanya ziara katika nchi za Ulaya kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano na kuondoa mkwaruzano.

Lakini chanzo cha tofauti kati ya Marekani na Ulaya ni kuwa, Marekani inashikilia siasa ya upande mmoja, na Ulaya inataka kuanzisha utaratibu wa ncha nyingi duniani; Marekani huichukulia Ulaya kuwa ni mfuasi wake, lakini nchi za Ulaya zinataka kuinua hadhi yao duniani. Tofauti hiyo imeonesha mikwaruzano kati ya maoni na maslahi ya aina mbili. Hivyo haijulikani kama ziara ya Bi. Rice itaweza kutimiza matumaini ya Marekani.

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-03