Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-04 15:27:30    
Hakuna msingi hata kidogo kwa Marekani kuingilia suala kati ya China na Ulaya

cri

Hivi karibu Marekani iliingilia suala kati ya China na Ulaya kuhusu Umoja wa Ulaya kuondoa vikwazo vya kuiuzia silaha China. Tarehe mosi, waziri wa mambo ya nje wa Marekani aliyeteuliwa hivi karibuni Condoleezza Rice alisema kuwa Marekani haitauachia Umoja wa Ulaya uondoe vikwazo vya kuiuzia silaha China bila kuushughulikia. Tarehe 2 bunge la Marekani lilipitisha azimio la kupinga Umoja wa Ulaya kuiuzia silaha China. Lakini hakuna msingi hata kidogo kwa Marekani kutia mkono kwenye suala linalokuwa tu kati ya Umoja wa Ulaya na China.

Marufuku ya kuiuzia silaha China ni matokeo ya miaka ya vita baridi vilivyoendelea kwa miaka 15, sasa suala hilo limepitwa na wakati, na limekuwa "kikwazo" katika maendeleo ya uhusiano wa kimkakati kati ya China na Umoja wa Ulaya. Mwezi Desemba mwaka jana, viongozi wa China na Uholanzi walipokutana, Umoja wa Ulaya ulionesha tumaini la kuondoa marufuku ya kuiuzia silaha China. Mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya Bw. Jose Manuel Barroso alisema, Umoja wa Ulaya utaharakisha utatuzi wa kuondoa marufuku hiyo. Hivi sasa nchi wanachama wengi wanaunga mkono kufuta marufuku hiyo. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Jack Straw mwezi uliopita pia alisema kuwa Umoja wa Ulaya unatazamiwa kuondoa amri hiyo katika miezi kadhaa ijayo.

Lakini, mazungumzo kuhusu kufuta amri ya kutoiuzia silaha China yalitia msumari moto kwenye kidonda cha Marekani. Hoja ya Marekani ni kuwa kama Umoja wa Ulaya ukiondoa amri hiyo, China itanunua silaha nyingi za kisasa kutoka Ulaya na kuleta hali mbaya kati ya China bara na Taiwan. Tokea mwaka jana kwa mara nyingi Marekani ilishinikiza Umoja wa Ulaya ikijaribu kukwamisha Umoja huo kuondoa amri ya kutoiuzia silaha China, na baadhi ya maofisa wa Marekani hata walisema kuwa iwapo Umoja wa Ulala unang'ng'ania kufuta amri hiyo, Marekani itachukua "hatua kali" kutokana na uamuzi huo na hata itasimamisha maingiliano ya sayansi na teknolojia katika mambo ya kijeshi na kusimamisha ushirikiano wa viwanda vya kijeshi kati ya Marekani ya Umoja wa Ulaya.

Onyo la Marekani ni kichekesho kitupu. Serikali ya China kwa mara nyingi ilitangaza kuwa lengo la China la kutaka Umoja wa Ulaya uondoe amri ya kutoiuzia silaha sio kwa ajili ya kununua silaha kutoka Ulaya, bali inaona amri hiyo hailingani na hali ilivyo sasa ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ulaya, na imekuwa kikwazo cha maendeleo hayo. Hili ni suala la kisiasa. Ukweli ni kwamba wanasiasa wengi wamesema, nchi zote za Ulaya zimeweka utaratibu mkali wa kuidhinisha uuzaji silaha nje ya nchi, hata amri hiyo ikiondolewa nchi hizo pia hazitaiuzia China silaha za kisasa. Mwakilishi mwandamizi anayeshughulikia mambo ya nje na usalama katika Umoja wa Ulaya Bw. Solana alisema, kuiuzia silaha China hakutaathiri hali ya wasiwasi kati ya China bara na Taiwan. Mtaalamu wa masuala ya China wa Chuo Kikuu cha George nchini Marekani Bw. David Sambo pia anaona kuwa kuondoa amri hiyo hakutasababisha biashara kubwa ya silaha.

Mazungumzo kati ya China na Ulaya yote ni ya haki na hayataathiri maslahi ya upande wa tatu. Kwa hiyo China na Ulaya hazitaki upande wa tatu uiambie China na Ulaya nini cha kufanya au namna ya kufanya. Bw. Solana pia alisema kuwa kuondoa amri ya kutoiuzia silaha China ni jambo la ndani la Umoja wa Ulaya. Nia halisi ya Marekani ya kupinga Umoja wa Ulaya kufuta amri ya kutoiuzia silaha China ni kukwamisha tu maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ulaya.

Watu wamezingatia kuwa Rice alifanya ziara barani Ulaya kuanzia tarehe 3. Habari zinasema kuwa jambo muhimu katika ajenda yake ni suala la kuondoa amri ya kutoiuzia silaha China. Vyombo vya habari vinasema, nia ya Marekani ya kupinga kuondoa amri haitaathiri chochote uamuzi wa Umoja wa Ulaya kuhusu suala hilo, na pia haitasaidia chochote kuboresha uhusiano kati ya Marekani na Ulaya, hasara ni ya Marekani tu.

Idhaa ya kiswahili 2005-02-04