Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-04 16:17:53    
Palestina na Israel zajitahidi kufanikisha mazungumzo kati ya wakuu wa nchi hizo mbili

cri

Palestina, Israel, Misri na Jordan tarehe 8 zitafanya mkutano wa wakuu wa nchi nne kuhusu amani ya mashariki ya kati huko Sharm El-Sherikh, Misri. Mwenyekiti wa mamlaka ya taifa ya Palestina Bw. Mahmood Abaas na waziri mkuu wa Israel Bw Ariel Sharon wote watahudhuria mkutano huo. Huu ni mkutano wa mara ya kwanza kukutana moja kwa moja kati ya viongozi wa Palestina na Israel tangu mwezi Oktoba mwaka 2000 huu ni muhimu sana kwa ajili ya kujenga upya imani, kurejesha mazungumzo ya amani na kuzindua tena mpango wa amani ya mashariki ya kati.

Ili kufanikisha mkutano huo, pande mbili za Palestina na Israel zimefanya juhudi za mfululizo, kuonesha urafiki kwa upande mwingine ili kuboresha uhusiano kati yao.

Siku za karibuni, hali ilitulia katika Palestina na Israel. Makundi mbalimbali yenye silaha ya Palestina kimsingi yametekeleza ahadi zao kwa mamlaka ya taifa ya Palestina na kusimamisha mashambulizi dhidi ya Israel. Wakati huo huo, mazungumzo ya raundi mpya ya maafikiano kati ya makundi mbalimbali ya Palestina yanafanyika nchini Misri. Waziri mkuu wa serikali ya Palestina Bw. Ahmed Qurei tarehe 3 alieleza kuwa juhudi za kusimamisha vita zilizofanywa na viongozi wapya wa Palestina ni za dhati. Hali ya hivi sasa inaonesha kuwa Palestina na Israel zinatazamiwa kutimiza amani ya kweli.

Israel ikiwa upande unaoongoza mgogoro kati ya Palestina na Israel, msimamo wake ni muhimu kwa ajili ya kutuliza uhusiano kati yao. Katika mazingira ambayo ilichukua hatua madhubuti za kutuliza mgogoro kati ya Palestina na Israel, baraza la mawaziri la usalama la Israel tarehe 3 liliitisha mkutano wa muda wa saa nne mjini Tel Aviv na kuamua kuwaachia huru wapalestina 900 waliotiwa nguvuni yaani kuwaachia huru wapalestina 500 kati ya wapalestina hao 900 mara tu baada ya mkutano wa wakuu wa tarehe 8, na kuwaachia huru wengine 400 baada ya miezi mitatu. Mkutano huo pia uliamua kuwa jeshi la Israel litaondoa kwanza jeshi lake kutoka mji Jericho, kando ya magharibi ya mto Jordan. Mkutano huo pia uliidhinisha uamuzi uliofanywa na jeshi la Israel hivi karibuni kuhusu kukubali kuunda kamati ya pamoja na Palestina, ili kusawazisha suala kuhusu Israel kuwasaka wanajeshi wa Palestina. Habari zinasema kuwa Israel imekubali kuwa kama wapalestina watatoa ahadi ya maandishi ya kutoishambulia Israel na kusalimisha silaha zao, basi Israel itasimamisha kuwasaka.

Lakini, maofisa wa Israel walisisitiza pia kuwa Palestina lazima ijibu hatua za kirafiki za Israel kwa vitendo halisi.

Kuhusu mkutano wa wakuu wa nchi nne za mashariki ya kati utakaofanyika tarehe 8, pande mbili za Palestina na Israel na jumuiya ya kimataifa zote zina matarajio makubwa. Waziri wa mambo ya mazungumzo wa Palestina Bw. Saeb Erekat na naibu waziri mkuu wa Israel Bw. Shimon Peres tarehe 3 walieleza matumaini yao kuwa viongozi wa nchi hizo mbili watafikia makubaliano ya kusimamisha vita kati yao katika kipindi cha mkutano huo.

Idhaa ya kiswahili 2005-02-04