Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-04 19:22:00    
Kukunja karatasi

cri

    Karatasi moja ya kawaida huweza kukunjwa na kuonekana kuwa mnyama mdogo anayeonekana kama yu hai, baada ya Bwana Liu Xiaoyi kuikunjakunja kwa mikono yake hodari. Vipepeo, mavunjajungu, samaki wa rangi ya dhahabu, mbuzi, tembo na swala hupendaza sana kutokana na kutengenezwa kwao kwa ufundi au kwa maumbo yao. Kwa vile ustadi wa Bwana Liu wa kukunja karatasi ni mkubwa sana, hivyo habari zake ziliandikwa katika kitabu cha Watu Maarufu wa Kimataifa tokeo la mwaka 1987-1988 kilichotungwa na Kampuni ya Uchapishaji ya Ulaya huko Uingereza.

    Bwana Liu alizaliwa katika familia ya kawaida mjini Yucheng kwenye jimbo la Shandong. Mama yake ni mwanamke wa kijijini, ingawa hajui kusoma wala kuandika, lakini ana mikono miwili myepesi, ana ufundi wa kukata karatasi, kukunja karatasi, kufuma vitambaa, na kutia rangi kwenye vitambaa. Bwana Liu aliathiriwa sana na mama yake. Tangu utotoni alipenda kutengeneza vikorokoro kwa kutumia iris ndogo za Kichina.

    Alipokuwa na umri wa miaka 8, Liu alikuja Beijing kusoma katika shule fulani ya msingi. Alipokuwa darasa la tatu alisuka chombo cha kuputia taka kwa kutumia waya, na kwa jalala hiyo alisifiwa na shule. Baada ya hapo alijifunza kuchora picha kwenye Kasri la Watoto. Mwaka 1965 alihitimu katika Shule ya Kati iliyoko chini ya uongozi wa Chuo Kikuu cha Sanaa ya Uchoraji, na baada ya kufaulu mtihani alijiunga na Chuo Kikuu cha Sanaa za Mikono na Sanaa ya Uchoraji na kuwa mwanafunzi katika kitivo cha upambaji.

    Baada ya kuhitimu alifanya kazi katika shirika moja la uchapishaji wa jarida akiwa mhariri wa sanaa ya uchoraji. Nyumbani, alipokuwa akimtunza mtoto wake, alianza kukunja vitu mbalimbali kwa kutuia karatasi badala ya iris ndogo za Kichina ambazo ni adimu kupatikana mjini Beijing. Baadaye akaanza kutafiti ufundi wa kukunja karatasi.

    Si rahisi kukunja karatasi zikawa sanamu za wadudu au wanyama wadogo wanaonekana kama wako hai. Ili kufaulu alifuga wanyama wadogo wengi kama vile samaki wa rangi ya dhahabu, kambakoche na kasa. Mwishowe akafanikiwa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-04