Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-08 19:42:30    
Vibarua wakulima "wayamudu" maisha ya utamaduni

cri
    Hali ambayo vijana wenye nguvu zaidi ya milioni 100 wanapitisha maisha yao kwa kucheza karata, kupiga soga na kulala tu baada ya kutoka kazini, ni hali isiyoweza kupuuzwa katika jamii yoyote bila kushughulikiwa. Kwa hiyo kuwapatia vijana hao waliotoka vijijini kuja kufanya kazi ya ujenzi mijini maisha ya utamaduni ili wasiachwe na jamii inayoendelea ni tatizo kubwa nchini China.

    Hivi karibuni, Wizara ya Utamaduni ya China na idara za utamaduni nchini China zilipeleka vitabu na sahani za video kwenye sehemu wanazofanya kazi, na Kundi la Nyimbo na Dansi la China lilionesha michezo yao kwa ajili yao, wasanii na wasomi walitoa mihadhara.

    Ili kuwawezesha vibarua wakulima kupata maisha ya utamaduni, Wizara ya Utamaduni imezitaka idara za utamaduni katika ngazi zote ziwahudumie vibarua wakulima na kuinua kiwango chao cha utamaduni katika siku wanapokuwa wakijenga miji.

    Katika hekaheka za kuwahudumia bure kiutamaduni vibarua wakulima, Jumba la Utamaduni la Chaoyang mjini Beijing liko mbele. Mwezi Novemba mwaka 2004 jumba hilo lilifungua jumba la kuonesha filamu, hilo ni jumba la kwanza mjini Beijing kwa ajili ya kuwaoneshea filamu vibarua wakulima, kila wiki jumba hili linawaonesha filamu vibarua wakulima 500 kwa muda wa saa mbili.

    Mapema miaka mitatu iliyopita jumba hilo lilikuwa na mpango wa kuwahudumia vibarua wakulima. Tarehe 5 Machi mwaka 2002, kwenye kiwanja mbele ya Jumba la Utamaduni la Chaoyang lilijengwa jukwaa la muda, vibarua wakulima 16 walicheza mchezo jinsi walivyofanya kazi kwa juhudi. Mchezo wao unawafikirisha watu kuwa "Wanakidhi maisha yetu kila kitu, lakini vipato vyao ni vidogo, na kazi yao ni nzito, hali yao ya maisha inasikitisha. Wao ndio wakarimu wa kutusaidia mahitaji yetu! Kazi yao yastahili kusifiwa!" Kutokana na fikra hizo hekaheka ya kuwahudumia vibaru wakulima utamaduni imeanzishwa ili kuwashukuru kwa mchango wao katika ujenzi wa miji. Mkuu wa Jumba la Utamaduni la Chaoyang Bw. Xu Wei alisema, jasho la vibarua wakulima kwa ajili ya ujenzi wa mji, na moyo wao wa kuvumilia shida unafaa kutambuliwa na kusifiwa na wakazi wa miji.

    Juhudi za Jumba la Utamaduni la Chaoyang zinasifiwa na ziliigwa na idara nyingi za utamaduni nchini China. Jumba hili kwa kushirikiana na idara nyingine lilifanya mashindano ya waimbaji vibarua wakulima, na liliwashirikisha watoto wa vibarua hao na watoto wa Beijing katika mashindano ya hotuba ya baada ya kusoma vitabu vizuri. Idara ya Utamaduni ya Beijing ilisaidia kwa kutoa gari la kuonesha filamu kwenye sehemu za ujenzi, hili ni gari la kwanza la kuwaonesha filamu vibarua wakulima mjini Beijing. Jumba la michezo ya sanaa mjini Beijing pia lilifungua mkahawa wa chai kwa ajili ya vibarua hao wanapokuwa likizoni, nao wanakunywa chai huku wakiburudika na maonesho ya michezo.

    Wizara ya Utamaduni imeweka mwaka 2005 kuwa ni "Mwaka wa Utamaduni Vijijini". Tuna uhakika kuwa "haki ya vibarua wakulima kufaidi utamaduni" hakika itahakikishwa zaidi katika mwaka huu.