Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-08 20:39:01    
Michezo ya mazoezi ya kujenga mwili

cri

Kampuni ya michezo ya mazoezi ya kujenga mwili ya CSI Bally ni kampuni yenye nguvu katika soko la michezo hiyo nchini China, ambayo ina vilabu vya kufanya mazoezi katika miji 9 nchini China. Naibu mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Wan Lihua ameshughulikia sekta hiyo kwa miaka mingi, akisema:

"Tumeona hali ya kuwafurahisha, China imeanza kuagiza njia mwafaka ya uendeshaji wa vilabu vya hali ya juu vya michezo hiyo ya Ulaya magharibi na Marekani. Vilabu vinapaswa kufikiri namna ya kuwaongoza watu kufanya kisayansi mazoezi hayo. Kwa kufanya hivyo, vilabu hivyo vitakuwa na ushindani katika soko la michezo huo.

Katika kipindi cha mwanzo cha kuanzishwa kwa sekta ya michezo ya mazoezi ya kujenga mwili, klabu moja iliwaandalia wateja wao mpango mmoja wa kufanya mazoezi hayo, lakini haikufuatilia tofauti kati yao katika sifa za afya na umri. Kuanzia mwaka 2002, wazo la kocha wa binafsi lilianza kutumika katika mazoezi ya kujenga miili. Mfumo huo kocha mmoja kumwongoza mtu mmoja umekaribishwa na watu.

Barani Ulaya na Marekani, vilabu kuwa na wataalam wa chakula chenye virutubisho, ni kigezo muhimu cha kupima sifa ya klabu moja. Lakini zamani vilabu vya kufanya mchezo huo vya China vilipuuza suala hilo. Sasa vilabu bora vya michezo hiyo pamoja na CSI Bally, Qingniao na Impulse vimeiga njia za nchi zilizoendelea na kuweka wataalam wa chakula.

Katika kipindi cha mwanzo cha kuanzisha sekta ya kufanya mazoezi ya michezo ya kujenga miili, mipango ya kufanya mchezo huo ya vilabu vingi vilitumia vipindi vya michezo shuleni. Kuanzia miaka ya 90, kadiri kufanya mchezo huo kwa kutumia oxygen kulivyochomoza duniani, China ilianza kuagiza masomo ya kufanya mchezo huo ya Ulaya na Marekani. Baada ya miaka kadhaa, katika msingi wa kuagiza utaalam kutoka Ulaya na Marekani, China ilitunga masomo yanayoambatana na umaalum wa wachina. Mwaka 2000, dada wa kufanya mazoezi ya michezo ya kujenga miili wa China Jiang Yong aliunganisha mchezo wa Wushu katika masomo ya kufanya mazoezi. Masomo hayo yalitumika katika sehemu nyingi duniani.

Uendeshaji wa maduka yenye mmiliki mmoja uliopamba moto barani Ulaya na Marekani, pia umetumika kwa miaka kadhaa nchini China. Hadi hivi sasa, asilimia 10 ya vilabu vya michezo ya mazoezi ya kujenga mwili vinaendeshwa kwa njia ya kuendesha vilabu vyenye mmiliki mmoja, ambayo inakaribishwa na makarani vijana. Naibu mkurugenzi wa kampuni ya CSI Bally Bw. Wan Lihua anasema:

"Hasa kwa wafanyabiashara wanaosafiri kwa ndege huku na huko duniani, njia ya uendeshaji wa vilabu vyenye mmiliki mmoja inaweza kutosheleza mahitaji yao. Kwa mfano, kampuni ya CSI Bally ina vilabu katika miji 9 nchini China, wafanyabiashara wanaweza kupewa huduma ya kufanya mazoezi ya michezo ya kujenga mwili katika miji hiyo. Kwa kuwa kampuni yetu inashirikiana na kampuni ya Bally ya Marekani na kampuni hiyo ya Marekani ina vilabu 430 nchini Marekani, kwa hiyo wafanyabiashara wanaokwenda nchini Marekani, pia wanaweza kupewa huduma hiyo."

Bila shaka, sekta hiyo ya michezo nchini China ina upungufu kuliko nchi zilizoendelea. Sasa vyombo na zana za vilabu nchini China hazina tofauti kuliko zile katika nchi za nje, lakini sifa za makocha wanaoshughulikia sekta hiyo ni za kiwango cha chini. Ingawa China imeendeleza sekta hiyo ya michezo kwa zaidi ya miaka 20, lakini hadi hivi sasa China bado haijaanzisha utaratibu wa kuidhinisha sifa za makocha, jambo ambalo limesababisha tofauti ya viwango cha makocha hao. Kwenye mkutano wa kimataifa wa michezo ya mazoezi ya kujenga mwili wa Beijing mwaka 2004, mwenyekiti wa chuo kikuu cha michezo na afya cha Asia Bw. Kenny Wong aliainisha kuwa, vilabu vya michezo ya mazoezi ya kujenga mwili vinahitaji makocha wenye sifa na kiwango cha juu. Sasa suala kubwa linalokabili sekta hiyo ya China ni viwango tofauti vya makocha. Kwa hiyo, sasa inapaswa kusawazisha soko la sekta hiyo nchini".

   

Kuhusu suala hilo, naibu mkurugenzi wa kituo cha kuanzisha maliasili ya nguvu za watu cha idara kuu ya michezo ya China Bi. Liu Tun anasema:

"China itatekeleza hatua kwa hatua utaratibu wa kuidhinisha makocha wa kufundisha watu wa kufanya mazoezi ya michezo ya kujenga mwili. Makocha watakuwa na nafasi ya kufanya kazi hiyo baada ya kufaulu mtihani wa ustadi wa sekta hiyo". Anaamini kuwa hatua hiyo itafanya soko la sekta hiyo liwe rasmi zaidi nchini China, ili raia wa China wapewe huduma bora zaidi michezo ya mazoezi ya kujenga mwili.

Idhaa ya kiswahili 2005-02-08