Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-16 18:04:39    
Wakulima wafaidike zaidi

cri

    Katibu mkuu wa Kamati ya Chama ya Beijing Bw. Liu Qi hivi karibuni alipokuwa kwenye mkuktano wa kazi za vitongoji vya Beijing alisema kuwa "kutilia maanani maendeleo ya vijijini, kuwashughulikia wakulima na kuunga mkono kilimo" na kutatua vilivyo masuala hayo matatu ni kazi isiyotakiwa kucheleweshwa, nguvu za kuunga mkono kilimo lazima ziimarishwe zaidi ili wakulima wapate faida halisi.

    Beijing ni mji mkubwa nchini China, kilimo kwenye viunga vilivyo karibu mji huo hakijastawishwa kama kinavyotakiwa. Maeneo kwenye viunga vya Beijing ni makubwa, maliasili ni nyingi na kuna nafasi kubwa ya kuendeleza kilimo. Mwaka 2004 ulikuwa ni mwaka ambao sera za kuwasaidia wakulima zilitolewa nyingi na wakulima walipata faida kubwa kuliko wakati wowote uliopita, thamani ilizozalishwa kwenye viunga vya Beijing hata ilifikia yuan bilioni 97, hili ni ongezeko la asilimia 15.5 kuliko mwaka uliotangulia, na ongezeko lake tupu lilikuwa asilimia 9.2 baada ya kuondoa bei iliyopandwa. Hata hivyo, tofauti ya kiuchumi kati ya mjini na vijijini bado haijapunguzwa.

    Bw. You Qi alisema, suala la kuwasaidia wakulima ni tatizo la msingi la kazi ya Chama na serikali, ni kazi muhimu kati ya kazi kuu za Chama kizima. Kazi ngumu na ya muhimu ya kutekeleza maendeleo ya kisayansi, kujenga jamii yenye maisha bora iko vijijini. Kwa hiyo inatupasa tutilie maanani maendeleo ya vijijini, kuwashughulikia wakulima na kuunga mkono kilimo. Kadiri ujenzi wa kisasa unavyoendelea mjini Beijing ndivyo nafasi ya maendeleo ya viungani mwa Beijing inavyokuwa muhimu zaidi katika uchumi wa Beijing. Bila kutatua vema tatizo la wakulima maendeleo ya viunga vya Beijing hayawezi kupatikana haraka, na mkakati wa maendeleo ya Beijing, lengo la kufanya michezo ya Olimpiki iwe ya "Beijing Mpya, na Olimpiki Mpya", pamoja na lengo la kujenga jamii ya upatanifu litakuwa vigumu kutimizwa.

    Bw. You Qi alisema kuwa Beijing ikiwa sehemu iliyoendelea kiuchumi imekiuka kizingiti na pato la mwenyeji kwa wastani limekuwa sawa na nchi zilizoendelea kiasi duniani, na Beijing imeingia katika kipindi cha "viwanda kusaidia kilimo, na ustawi wa mjini kusukuma maendeleo ya vijijini". Alisisitiza kuwa uwezo wa mjini wa kusukuma maendeleo ya vijijini unapaswa kuimarishwa zaidi na ustawi wa viunga vya Beijing uyasaidie maendeleo ya mjini, matumizi ya fedha za serikali ya Beijing yanahitaji kurekebishwa, fedha za umma zitumike zaidi vijijini, na kwa sera zenye fursa maalumu kuongeza juhudi za kusaidia sekta ya kilimo. Pamoja na hayo baadhi ya mashirika yahimizwe kuhamia viungani na kuhamasisha baadhi ya idara za mjini kama hospitali, na shule kuhamia viungani na kwa kila njia kusaidia ustawi wa viungani. Zaidi ya hayo, mji na vitongoji vinapaswa kusaidiana katika nyenzo, masoko ili kusukuma mbele maendeleo ya pande zote ya uchumi wa Beijing.

    Kutokana na takwimu, mwaka jana mitaji ya serikali ya Beijing ilitenga yuan bilioni 2.6 na bilioni 2 katika matumizi ya ujenzi wa miundo mbinu na maendeleo ya jamii, hili ni ongezeko la 1.4 na 1.1. Uwiano wa kiasi cha uwekezaji wa serikali ya mji kati ya mjini na viungani mwaka 2004 ulikuwa 6 kwa 4 badala ya 8 kwa 2 mwaka 2003, na mwaka huu uwiano huo utarekebishwa na kuwa nusu kwa nusu. Bw. You Qi alisisitiza kuwa marekebisho ya kiasi cha matumizi ya fedha kati ya mjini na viungani lazima yafanywe, na kuongeza mafanikio ya uwekezaji, na kukusanya nguvu kwenye utatuzi wa tatizo moja au matatizo mawili ambayo yanawatatiza zaidi wakulima, na kuwapatia wakulima faida za kilimo cha kitaalamu.

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-16