Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-16 18:26:05    
Namna ya kupika nyama ya nguruwe yenye ladha tamu na siki

cri

Mahitaji

Nyama ya nguruwe gramu 240, mananasi yaliyokwisha kukatwa kuwa vipande vidogo, pilipili mboga moja, nusu ya kitunguu kimoja, nusu ya yai, wanga vijiko vinne, kiasi kidogo cha mafuta, chumvi 1/3 ya kijiko, sukari 1/4 kijiko, siki nusu ya kikombe, maji ya wanga kijiko kimoja

Njia

1. Kata nyama ya nguruwe iwe vipande vyenye mraba wa urefu wa sm 2 na upana wa sm 2, koroga yai na tia chumvi, sukari, tia vipande vya nyama ya nguruwe ndani ya mchanganyiko huo, halafu tia wanga na koroga.

2. tia mafuta ndani ya sufuria mpaka yawe na joto la nyuzi 60 hivi tia vipande vya nyama ya nguruwe ndani ya sufuria, mpaka rangi inapokuwa ya hudhurungi, na vipakue.

3. pasha moto tena, tia pilipili ya mboga na vitunguu korogakoroga, tia vipande vya nyama ya nguruwe na mananasi na mimina mchuzi uliochanganywa na sukari na siki, chemsha, tia chumvi halafu mimina maji ya wanga, koroga na kupakua, kitoweo hiki sasa kiko tayari