Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-16 18:36:07    
Utafiti wa "Super mahindi" wapata mafanikio makubwa

cri
    Baada ya kufanya utafiti na majaribio kwa mara nyingi, wanasayansi wa kilimo wa China wamefanikiwa kuotesha "Supa mahindi". Zao hilo bora lenye uzalishaji mkubwa linaweza kukabiliana na maafa mengi ya kimaumbile pamoja na uharibifu wa wadudu, na linaweza kuleta ongezeko la uzalishaji wa chakula kwa China. "Super mahindi" ni mradi mwingine mkubwa wa utafiti wa sayansi katika sekta ya kilimo kwa kufuata "Super mpunga" hapa nchini.

    Kutokana na kufuata mpango wa utafiti wa miradi muhimu uliotangazwa na serikali ya Beijing tarehe 11 mwezi Januari, ingawa mbegu ya "Super mahindi" itatolewa rasmi katika miaka mitatu ijayo, lakini mahindi mapya yaliyooteshwa nchini China yamekuwa karibu sana na lengo la mahindi ya aina mpya yajulikanayo kwa jina la "Super mahindi" na yameongoza duniani.

    Bw. Zhao Jiuran, ambaye ni mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa mahindi ya chuo cha sayansi ya kilimo na misitu cha Beijing, alisema kuwa mwaka 2004 ofisi hiyo ilipata aina 4 mpya za mbegu za mihindi inayoweza kuzaa mahindi zaidi ya tani 13.5 kwa hekta, kiasi ambacho ni pungufu kidogo tu na lengo la uzalishaji wa "Super mahindi" ambalo ni tani 15 kwa hekta, licha ya hayo malengo mengine kama ya ubora na kuvumilia maafa pia yanakaribia ya "Super mahindi". Mahindi ni zao la pili kwa ukubwa nchini China, ambalo kila mwaka linalimwa katika mashamba hekta milioni 26.7 hivi, lakini uzalishaji wake ni chini ya tani 6 kwa hekta, ingawa baadhi ya mashamba yalizalisha mahindi mengi, lakini hali hiyo siyo katika kila mwaka.

    Kwa kufikiria hali tofauti kati ya sehemu nyingine na ambazo yalifanyika majaribio ya uzalishaji wa "Super mahindi", kwa uchache kabisa ongezeko la uzalishaji kutokana na kutumia mbegu za "Super mahindi" litazidi tani 2.25 kwa hekta. Ikiwa hekta milioni 2.67 za mashamba zitapandwa mbegu za "Super mahindi", ongezeko la uzalishaji wa mahindi nchini litafikia tani milioni 6, kiasi hicho ni kama ongezeko la mashamba kiasi cha hekta milioni 1.China ikiwa nchi kubwa katika uzalishaji wa chakula, inazingatia sana utafiti wa aina mpya za mbegu za mahindi.

    Katika mkutano wa majadiliano kuhusu mpango wa zao la "Super mahindi", wataalam wa kilimo waliona kuwa kiwango cha teknolojia ya zao la "Super mahindi" ni cha kisasa kabisa, China imekuwa na hakimiliki kamili kuhusu zao hilo na imehesabiwa kuwa ni uvumbuzi mkubwa wa mradi mpya wa teknolojia. Katika hali ya kupungua kwa maeneo ya mashamba, ukulima wa zao la "Super mahindi" utakuwa muhimu katika utafiti na matumizi ya teknolojia mpya.

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-16