Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-17 15:46:33    
Utekelezaji wa Mpango wa Upande Mmoja wa Sharon Wavuka Kikwazo

cri

Tarehe 16 bunge la Israel lilipitisha "sheria ya kuwafidia wakazi Wayahudi wanaohamishwa kutoka kwenye makazi". Sheria hiyo imesaidia kisheria utekelezaji wa mpango wa upande mmoja wa Sharon kwa kuondoa kikwazo kikubwa.

Kutokana na kuwa watu wa mrengo wa kulia walikuwa wanajitahidi kupinga mpango wa upande mmoja wa Sharon, sheria hiyo ambayo inahusiana moja kwa moja na mpango huo ilikuwa tatizo linalobishaniwa sana katika historia ya nchi hiyo. Tokea mwezi Septemba mwaka jana sheria hiyo ilipotungwa, wapinzani hao walizuia kadiri wawezavyo sheria hiyo isipitishwe katika bunge.

Kabla ya kuipigia kura kwa mara ya mwisho sheria hiyo katika bunge, wapinzani waliendelea "kupinga kikaidi" na kutoa mapendekezo mengi yakiwa ni pamoja na "mpango wa upande mmoja upigiwe kura kitaifa", lakini yalikataliwa. Mwishowe sheria hiyo ilipitishwa kwa kura 59 dhidi ya 40 katika bunge.

Kwa mujibu wa mpango wa upande mmoja, kabla ya mwishoni mwa mwaka huu Israel itawahamisha wakazi Wayahudi 8,000 wa sehemu 21 katika ukanda wa Gaza na sehemu 4 za makazi ya Wayahudi kwenye ukingo wa magharibi wa Mto Jordan. "sheria ya kuwafidia wakazi Wayahudi wanaohamishwa" imeipa serikali ya Israel madaraka ya kuchukua hatua ndani ya muda wa miezi mitano, na kutoa fidia jumla ya dola za Kimarekani bilioni moja kwa wakazi na mashirika katika sehemu hizo ili kuwasaidia watu hao kupata makazi, kazi mpya na kuwasomesha watoto. Kwa makadirio, kila familia inaweza kupata fidia kiasi cha dola za Kimarekani laki 4, zikiwa pamoja na gharama nyingine, mpango huo wa upande mmoja jumla utagharimu dola za Kimarekani bilioni 1.6.

Vyombo vya habari vinaona kuwa kutokana na sheria hiyo kupitishwa, mpango wa upande mmoja wa Sharon umekuwa bayana. Kabla ya utekelezaji wa sheria hiyo serikali inahitaji tu kukubaliwa na baraza la serikali. Kwa hiyo, tarehe 16 naibu waziri mkuu Shimon Peres anayeshughulikia utekelezaji wa mpango wa upande mmoja ameitangazia dunia akionesha dhamira ya kuwahamisha makazi ya Wayahudi. Imefahamika kuwa tarehe 20 baraza la serikali ya Israel itapiga kura kuiruhusu serikali, wakati huo serikali itapewa haki na kuanza kutekeleza mpango wa upande mmoja. Kutokana na mpango wa serikali, shughuli za kuwahamisha makazi ya Wayahudi zitaanza rasmi katika mwezi Julai, na zitaendelea kwa wiki 12.

Lakini vyombo vya habari pia vinaona kuwa pamoja na serikali kuondoa jeshi lake kutoka sehemu ya Gaza inaendelea kujenga "ukuta wa utenganisho" ikijaribu kuleta hali ya "maji yaliyomwagika" kuikalia ardhi ya Palestina. Kutokana na ramani ya ukuta iliyorekebishwa hivi karibuni, baadhi ya sehemu za makazi ya Wayahudi zimekatwa kuwa upande wa Israel, baraza la serikali litakapopiga kura kuhusu mpango wa upande mmoja ramani hiyo ya "ukuta wa utenganisho" pia itapigwa kura.

Wachambuzi wanaona kuwa ujanja wa Sharon kupanga mambo hayo mawili kupigiwa kura katika siku moja ni kutaka kukwepa laana ya kimataifa kuhusu ujenzi wa "ukuta wa utenganisho" uliorekebishwa kwa kuondoa jeshi lake kutoka Gaza.

Idhaa ya kiswahili 2005-02-17