Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-17 15:54:15    
Mazishi yenye mtindo dhahiri wa kisiasa ya Bw. Rafik Hariri

cri

    Mazishi ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Bw. Rafik Hariri aliyeuawa hivi karibuni yalifanyika jana huko Beruit, mji mkuu wa nchi hiyo. Wanasiasa mashuhuri wa nchi mbalimbali na jumuiya za kimataifa, maelfu ya waungaji mkono wake na raia wa kawaida walihudhuria mazishi hayo. Wachambuzi wanaona kuwa, mazishi makubwa kama hayo si kama tu yameonesha heshima yake, bali pia yamefanya watu kufikiria kwa kina kuhusu uhusiano maalum kati ya Lebanon na Syria na hali ya nchini Lebanon katika siku za baadaye.

    Mazishi hayo yana umaalum wa aina tatu. Ya kwanza, rais wa Lebanon na waziri mkuu wa nchi hiyo hawakuhudhuria mazishi hayo. Hiyo inaonesha kuwa migogoro kati ya jamaa wa Bw. Hariri na serikali ya nchi hiyo imekuwa mikubwa zaidi. Kabla ya hapo, jamaa wa Bw. Hariri walikataa pendekezo la serikali hiyo la kumfanyia mazishi ya kiserikali na kushikilia kufanya mazishi ya kawaida. pili, wanasiasa wengi wa nchi za nje walihudhuria mazishi yake, hiyo inaonesha hadhi muhimu ya Bw. Hariri nchini humo. tatu, mazishi hayo dhahiri yalikuwa na maana ya kupinga Syria, baadhi ya watu waliohudhuria mazishi hayo walibeba mabango na kupiga makelele ya kuipinga Syria, na kuilaani Syria lazima iwajibike na kifo cha Bw. Hariri na kuhimiza jeshi la Syria kuondoka kutoka nchini Lebanon.

    Bw. Hariri aliwahi kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo kwa mara tano kuanzia mwaka 1992, na kusifiwa kuwa ni mhandisi wa ukarabati wa Lebanon baada ya vita. Kuuawa kwake kunafikiriwa kuwa ni tukio kubwa kabisa la kisiasa tangu kukomeshwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo mwaka 1990. kutokana na tukio hilo, jamii nzima ya nchi hiyo imevurugika, migongano ya ndani imezidi kuwa mikubwa, hali ya usalama nchini humo imeathiriwa vibaya na watalii wa nje wanaondoka nchini kwa haraka. Aidha, tukio hilo limefuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa taarifa kulaani tukio hilo. Marekani ilitangaza kumwita nyumbani balozi wa Marekani nchini Syria, na uhusiano kati ya Marekani na Syria umekuwa mbaya zaidi. Rais Chirac wa Ufaransa alitaka uchunguzi wa kimataifa ufanyike kuhusu tukio hilo, lakini pendekezo hilo limepingwa na serikali ya Lebanon.

    Tukio hilo pia limeleta lawama kubwa kwa Syria kutokana na jeshi lake kuwepo nchini Lebanon. Hivi sasa Syria inakabilana na shinikizo kubwa la kuondoa jeshi lake nchini Lebanon kutoka nchini na jumuiya za kimataifa. Wachambuzi wanaona kuwa, ingawa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Rice alitangaza kuwa hivi sasa Marekani haitaulaani upande wowote kuwajibika na tukio hilo, lakini kitendo cha Marekani kumwita nyumbani balozi wake nchini Syria kimeonesha maoni yake kuwa Syria inahusika na tukio la kuuawa kwa Bw. Hariri. Kitendo hicho kina lengo la kuweka zaidi shinikio kwa Syria ili kuilazimisha nchi hiyo kuondoa jeshi lake kutoka nchini Lebanon, ili kuvunja uhusiano kati ya Syria na Lebanon na kuitenga Syria. Lakini wachambuzi pia wanaona kuwa, kama tukio hilo halikutokea, chini ya shinikizo kubwa kutoka jumuiya ya kimataifa, Syria pia itaondoa jeshi lake nchini Lebanon. Lakini baada ya tukio hilo kutokea, hali ya nchini Lebanon huenda itakuwa na wasiwasi zaidi.

    Tahadhari inayostahili kuchukuliwa ni kuwa, migongano ya ndani ya Lebanon iliyozidi kuwa mikubwa italeta fursa kwa nchi za magharibi kuingilia tena mambo ya ndani ya Lebanon. Migongano ya kidini na kikabila nchini Lebanon ni yenye utatanishi mkubwa, na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo vilivyodumu kwa miaka 10 vilifanya nchi hiyo kuwa sehemu ya ushindani kwa nchi kubwa za kikanda na nchi za magharibi. Mwaka 1989, pande mbalimbali za nchi hiyo zilifikia makubaliano kuhusu suala la ugawaji wa madaraka na jeshi la Syria nchini humo, hali hiyo ilitoa nafasi nzuri kwa nchi hiyo kufanya ukarabati baada ya vita. Lakini, baada ya tukio hilo kutokea, wachambuzi wengi wana wasiwasi mkubwa zaidi kuwa vurugu zitalipuka tena nchini humo, na kufanya Lebanon iwe tena sehemu ya ushindani wa nchi kubwa za kikanda na duniani.

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-17