Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-18 16:20:25    
Wagonjwa wa Ukimwi wajiokoa wenyewe

cri

Karibu na mji wa Linfen mkoani Shanxi kuna mahali paitwapo "Ghuba ya Kijani". Huko wagonjwa wa Ukimwi wanaishi kwa furaha kama watu wengine.

Asilimia 80 ya wagonjwa wa Ukimwi mkoani Shanxi wako katika sehemu ya kusini mkoani humo. Katika mazingira ambayo hakuna nyumba, wataalamu wala zana za matibabu Hospitali ya Magonjwa ya Kuambukiza mjini Linfen ilijitayarisha fedha yuan milioni 1.5 ilikodi ardi yenye eneo la hekta 60 na kujenga sehemu maalumu ya wagonjwa wa Ukimwi, sehemu hiyo imepewa jina la "Ghuba ya Kijani". Tokea tarehe 24 Julai mwaka jana wagonjwa 20 waliwahi kuishi huko.

"Ghuba ya Kijani" ina kitengo cha matibabu, kitengo cha huduma za wagonjwa na ardhi ya kilimo. Katika kitengo cha matibabu kuna wadi na nyumba za kusomea, kucheza michezo na kuangalia picha za VCD. Ardhi ya kilimo ina eneo la hekta 46, mazao yanayolimwa na wagonjwa ni mahindi, alizeti, mboga na maua, mavuno yanatumika kusaidia maisha ya wagonjwa.

Katika "Ghuba ya Kijani", wagonjwa licha ya kupata ahueni pia wanapata furaha na nia ya kuishi.