Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-18 19:44:30    
Ngoma Katika Vyombo vya Kale

cri

    Kimoja miongoni mwa vitu vilivyopata zawadi kwenye maonyesho ya vitu vya kale vinavyohusu historia ya ngoma za Kichina yaliyofanya jijini Beijing, spring 1989, ni chungu cha udongo chenye umri wa miaka 5,000 cha Zama Mpya ya Mawe. Katika ukingo wake wa ndani kuna makundi matatu ya wachezangoma watano watano walioshikana mikono waliochorwa kwenye mabombwe ya maua-mfano wa kale wa uchezaji ngoma ambao haujapata kuonekana nchini China.

    Ngoma kama fani ya sanaa ya maonyesho ya Kichina inaweza kufuatiliwa historia yake tangu zama za jamii ya kitumwa. Hekaya zinaeleza kwamba Mfalme Jie ambaye ni mtawala wa mwisho wa Enzi ya Xia, alikusanya kundi la wasichana wachezangoma 30,000 kwa ajili ya kumstarehesha, na inafahamika kwamba Enzi ya Zhou ya Magharibi (1066-771 K.K.), watoto wa familia za makabaila walianza kufundishwa misingi ya kuimba na kucheza ngoma.

    Kifaa kingine cha kale zaidi katika maonyesho hayo kulikuwa mfuniko wa kasha lililopakwa rangi ngumu inyong'aa wa kipindi cha wasichana 11 wachezaji ngoma waliovaa nguo za mikono mirefu zenye viuno vyembamba. Watatu miongoni mwao wanaonekana wakifanya mazoezi ya muondoko wa kuinama na mwanamke mmoja waliyekunja mkono wa nguo yake na kushika mjeledi kama anawafunza wale wengine wawili.

    Enzi za Han (206K.K.-220 B.K.) na Tang (618B.K.-907B.K.) zilikuwa vipindi viwili vya mafanikio ya fasihi na sanaa za kale za China ikiwemo ngoma. Vipindi hivyo viwili vilikuwa vya mafanikio makubwa na nguvu na kulikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara kati ya makabila yaliyomo nchini na vilevile baina ya China na nchi za nje. Mawasiliano hayo yamesaidia sana kukuza ngoma za kichina na kutajirisha sana maudhui yake. Matokeo yake ni kujichomoza kwa mitindo mbalimbali mizuri ya ngoma. Kwa mujibu wa kumbukumbu za kihistoria, Enzi ya Han iliunda Baraza la Muziki ili kuandikisha na kufunza wanamuziki na wachezangoma, na familia nyingi za tabaka tawala zilikuwa na vikundi vyao binafsi vya ngoma na nyimbo.

    Maonyesho mbalimbali yaliyokuwa na aina zote za sanaa za jadi, kama vile kuimba na kucheza ngoma na sarakasi yalikuwa maarufu sana Enzi ya Han. Wakati vikundi vya ujumbe rasmi kutoka kwenye makabila ncini na nchi za nje vilipofanya ziara zao katika mji mkuu wa China, Mfalme Wu Di alikuwa akiwaburudisha kwa vikundi vikubwa vya kupendeza vya wasanii waliobobea-mwenendo huo uliendelea kwa muda wa miaka 60.

    Enzi ya Tang, kulianzishwa taasisi tatu za kiserikali kwa ajili ya kuendeleza shughuli za muziki na ngoma. Taasisi hizo ni Jiaofang, Liyuan na Taichangsi. Taasisi hizo zilikuwa na wasanii wa kupigwa mfano ambao walichaguliwa ili kutoa mafunzo kwa wasanii wapya kwa mpango maalumu. Wahitimu kutoka taasisi hizo waliweza kusambazwa nchi nzima kuwa ama wachezaji rasmi wa kiserikali, watoaji burudani kwenye kambi za jeshi au wasanii binafsi ambao waliwaburudisha matajiri na familia za kiutawala majumbani mwao. Enzi ya Tang, muziki na ngoma havikuwa vitu vya lazima kwenye sherehe na dhifa za kitaifa tu bali pia viliweza kuonyeshwa hadharani mbele ya msafara wa watawala walipokuwa wakitembea mitaani. Kusema kweli, sanaa hizo ziligawanywa katika makundi mengi zaidi.

    Mchongo mmoja wa mawe wa Enzi ya Han ulionyesha sehemu nne za matukio ya sanaa kwenye karamu (tazama picha ya tatu). Kwenye sehemu ya juu ya mkono wa kulia kuliweza kuonekana wanaume wawili mmoja akicheza mipira za mwingine akicheza na upanga kwenye mkono wake wa kulia na jagi likitulia kwenye kiko cha mkono wa kushoto. Chini yao ni msichana mwenye kiuno chembamba na nywele zilizofungwa matita mawili akicheza ngoma. Huku akipepea kitambaa kirefu cha hariri, kichwa chake amekigeuza nyuma mkabala wa mwenzake aliyekuwa nyuma yake aliyekuwa akipiga kayamba. Sehemu ya chini, kushoto ya mchongo huo, inawaonyesha wanamuziki wawili wakiwafuasa wachezaji kwa kupuliza nzumari na kupiga ngoma. Juu yao, upande wa kushoto wanaonekana watu wawili wakinywa pombe na kufurahia uhondo wa onyesho.

    Wakati wa kilele cha ufanisi wa Enzi ya Tang, dini ya Kibudhaa ilikuwa na nguvu sana nchini China na iliathiri sanaa kwa ujumla na hatimaye ikajipenyeza kwenye ngoma. Ushahidi wake upo kwenye michoro mingi ya kutani katika Mpango ya Mogao yaliyopo Dunhuang jimboni Gansu. Moja ya nakili zake iliyokuwa na jina la "Muziki na Dansi Kutoka Kwenye Ardhi Takatifu ya Buddha Anayeponya" ilikuwa moja ya vivutio vya maonyesho hayo. Mchoro huo uliotanda kwa urefu wa mita 4.18 ulihusu ngano ya kidini inayomuonyesha malaika wa mbinguni ambaye ni mchezaji akipiga pipa kinyumenyume. Jambo la kufurahisha ni kwamba mchezaji huyo na miondoko mingine ya ngoma iliyoonyeshwa kwenye mchoro huo wa ukutani ilikiandishi Kikundi cha nyimbo na Ngoma cha Gansu kuweza kubuni kwa mafanikio ya hali ya juu "Mtindo wa Dunhuang" wa kucheza ngoma.

    Enzi ya Song (960-1279), opera ilianza kuchukua nafasi ya ngoma kama sanaa ya maonyesho ya Kichina iliyotamalaki majukwaa. Matokeo yake ni kwamba wachezaji ngoma wengi maarufu wa kale walitokomea ingawa baadhi ya mbinu zao zilirithiwa na opera ili kuwakilisha wahusika mbalimbali.

    Tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China mwaka 1949, mkazo umekuwa ukitiwa kwenye ngoma za Kichina. Katika miaka 40 iliyopita, watafiti wamesafiri sehemu mbalimbali nchini ili kukusanya data zitakazowasaidia kutoka kwenye kasri za wafalme, mahekalu, makaburi ya kale na maneno mengine. Mnamo mwaka 1987, Taasisi ya Utafiti wa Sanaa za Kichina ilianza kutayarisha kitabu kijulikanacho kwa jina la "Historia ya Ngoma za Kichina katika Picha" chini ya uhariri wa Dong Xijiu na Liu Junxiang. Picha zilizokuwa kwenye maonyesho hayo zilichukuliwa kutoka kwenye kitabu hicho ambacho bado kinatayarishwa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-19