Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-18 20:48:27    
Mchina azungumzia SAFARI ya Mbuga ya Masai Mara nchini Kenya

cri

    Neno la SAFARI linatumika katika nchi nyingi za Afrika Mashariki, watu wakienda Kenya wataliona limeandikwa kwenye magari yote ya utalii nchini humo. Kama nchi nyingine nyingi za Afrika ya Mashariki, Kenya ina maliasili nyingi za wanyama wa porini na mazingira mazuri ya kimaumbile. Kila mwaka, mamilioni ya watalii wanakwenda nchi hiyo kufanya utalii.

    Katika Kampuni inayoshughulikia biashara ya vifaa vya ofisi kwenye mtaa wa Zhong Guancun wa Beijing, China, mwandishi wetu wa habari alimhoji Bw. Dai Song aliyerudi China hivi karibuni baada ya kufanya utalii barani Afrika. Akizungumzia safari yake, Bw. Dai alichangamka sana, na kumwonesha mwandishi wetu picha zake alipokuwa Afrika. Bw. Dai alikumbuka safari yake katika Mbuga ya Masai Mara nchini Kenya akisema:

    "Mbuga ya hifadhi ya wanyama ya Masai Mara iliyoko kwenye mpaka wa Kusini Magharibi ya Kenya na Tanzania iko umbali wa kilomita 340 kutoka Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Kuna njia mbili za kwenda Masai Mara kutoka Nairobi: kwa gari la utalii na ndege ndogo. Nalichagua kwenda kwa ndege ndogo kutokana na kutokuwa na muda wa kutosha.

    Bw. Dai alisema kuwa, ilimchukua muda usiozidi saa moja kwa ndege kufika kwenye Mbuga ya Masai Mara kutoka Nairobi. Yeye pamoja na watalii wengine walikaa kwenye hoteli ya Mara Safari Club yenye mtindo maalum wa hema. Hoteli hiyo iko kwenye kando ya mto ulioko upande magharibi ya Masai Mara. Ndani yake, mitindo ya kisasa na kimaumbile inaendana vizuri, na zana zilizokamilika zinawahudumia vizuri watalii. Bw. Dai anasema:

    "Siku ya pili, saa kumi asubuhi, mvulana mmoja alinisalimia mlangoni na kuniletea chakula cha maziwa, kahawa, sukari na biskuti, aliniambia kuwa gari liko tayari kunichukua kwenda kuangalia wanyama kwa kupanda kwenye puto linaloelea."

    Baada ya saa moja, puto la hewa ya joto nilikokaa liliruka, na tuliweza kuona mandhari nzuri kutoka angani. Ilikuwa ni mapema asubuhi na kulikuwa kimya sana, lakini baadhi ya wanyama walikuwa wameanza kutafuta chakula. Baada ya muda wa saa moja,safari yetu ikamalizika, wakati huo, wahudumu walikuwa wametuandalia kifungua kinywa kitamu sana. Kweli ni jambo la kufurahisha sana kuburudika kwa chakula kitamu baada ya kuona madhari nzuri. Mwezi Agosti hadi Oktoba kila mwaka ni wakati mzuri kutembelea mguba za wanyama kwa kutumia puto. Wakati huo, makundi makubwa ya wanyama wanahamia Masai Mara kutoka Mbuga ya wanyama ya Serengeti nchini Tanzania, ambapo mamilioni ya kongoni walikuwa wanavuka Mto Mara na kuelekea mbuga ya wanyama ya Masai Mara, mandhari nzuri iliyoje! Huwezi kuamini bila ya kuona. Bw. Dai Song anasema:

    "Baada ya kupata kifungua kinywa,tulikwenda kwa gari hotelini kwetu kwa kupita mbugani. Njiani, tuliona wanyama watanowakubwa maarufu wa aina tano wa Afrika wakiwemo ndovu, vifaru, simba, nyati na chui."

    Asubuhi ya majira ya kiangazi, mwanga wa jua ulikuwa ukimulika kwenye mbuga mkubwa, na tuliweza kuona makundi mbalimbali ya wanyama wakila majani hata sauti zao za kutafuna zilikuwa zikisikika, lakini ghafla walitimua mbio na kutawanyika, kumbe simba mmoja alikuwa anapita, lakini simba hakuwajali hata kidogo, wala hakusimama ili kuweze kupiga picha, labda ameshiba sana.

    Saa tatu asubuhi, jua lilikuwa kali sana, liliwafanya wanyama wapumzike vichakani, tukarudi hotelini. Tukiwa njiani ya kurudi hoteli, tuliwatembelea wamasai kadhaa. Wamasai wanaume walivaa vitambaa vyekundu vyenye mistari myeusi, na wanawake walivaa mapambo mbalimbali kichwani. Walituongoza kutembelea nyumba yao iliyojengwa kwa miti na udongo, na kutualika kunywa vinywaji vilivyotengenezwa kwa kuchanganya damu ya ng'ombe na maziwa. Baadaye walianza kucheza ngoma kwa furaha kubwa.

    "Saa kumi hivi alasiri, tulianza safari mpya ya kuangalia wanyama. Kwenye safari hiyo tuliona wanyama wengi zaidi, pamoja na duma. Ingawa duma hayupo kati ya wanyama maarufu wa aina tano, lakini ana mwili wenye nguvu, mnyumbufu na ana kasi kubwa sana, huyo ni mnyama niliyempenda zaidi. Watu wanaweza kuhisi uzuri wa maumbile wakati wanapotafuta wanyama mbalimbali porini."

    Katika safari ya kurudi hoteli, dereva alituambia kuwa, kama tunapenda tutaweza tukaenda kwa gari usiku kuangalia wanyama kwa kutumia kifaa maalum cha kutizamia usiku kutafuta wanyama wasiotembelea mchana. Aidha, Hoteli itawaandalia watalii chakula cha usiku mbugani, na watu wanaweza kula chakula cha usiku chenye mtindo wa Uingereza huku wakitazama ngoma nzuri wanazocheza wamasai.

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-18