Gazeti la Joongang Ilbo la Korea ya kaskazini leo limemkariri naibu mjumbe wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa Bwana Han Song-ryol akisema kuwa, ikiwa Marekani inaahidi kuishi pamoja na Korea ya kaskazini na kutoingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo, Korea ya kaskazini itapenda kurudi tena kwenye mazungumzo ya aina yote kuhusu suala la nyuklia la peninsula la Korea ikiwa ni pamoja na mazungumzo ya pande sita.
Bwana Han Song-ryol alisema kuwa, huu ni msimamo wa Korea ya kaskazini katika taarifa yake iliyotolewa tarehe 10 mwezi huu. Alisema kuwa, Korea ya kaskazini haitachagua kurudi nyuma, lakini ikiwa Marekani itaacha sera ya uhasama dhidi ya nchi yake, basi Korea ya kaskazini pia itaacha sera ya kuipinga Marekani.
Ilipofika mwezi wa Juni mwaka jana, nchi sita China, Korea ya kaskazini, Marekani, Korea ya kusini, Russia na Japan zilikuwa zimefanya mazungumzo mara tatu kuhusu utatuzi wa amani wa suala la nyuklia la peninsula la Korea. Tarehe 10 mwezi huu, wizara ya mambo ya nje ya Korea ya kaskazini ilitoa taarifa ikisema kuwa haina budi kusimamisha mazungumzo ya pande sita, ikisema kuwa, nchi hiyo imeshatengeneza silaha za nyuklia ya kujihami kutokana na sera ya uhasama ya Marekani dhidi ya nchi hiyo.
|