Ghasia kubwa jana zilizuka kati ya wafanyabiashara wadogo wa Tunduma na wenzao wa Nakonde Zambia mpakani mwa Tanzania na nchi hiyo.
Katika vurugu hizo, watu walirushiana mawe na bidhaa mbalimbali katika soko hilo la mpakani na ambapo bidhaa nyingine zilichomwa moto.
Habari zinasema kuwa mashambulizi hayo yanafuatia kukamatwa kwa Watanzania 60 waliokwenda upande wa Zambia mapema wiki hii.
|