Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-19 19:35:00    
Dar es Salaam-Serikali ya Sweden yatoa msaada wa kupambana na ukimwi kwa Tanzania

cri

    Katibu mkuu wa wizara ya afya ya Tanzania Bw. Grey Mgonja alisema kuwa, Serikali ya Sweden imeipatia Tanzania dola za kimarekani milioni 2.1 zitakazotumika kununulia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa ukimwi.

    Bw. Mgonja baada ya kutia saini mkataba na balozi wa Sweden nchini Tanzania juu ya msaada huo, alisema kuwa fedha hizo pia zitatumika kuboresha huduma za wagonjwa wa ukimwi.

    Naye balozi wa Sweden Bw. Torvald Akesson, alisema serikali ya nchi yake imetoa msaada huo kwa kutambua umuhimu wa kuwasaidia waathirika wa ukimwi.