Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-19 21:12:07    
 Khartoum-Mjumbe wa serikali ya China afanya mazungumzo na viongozi wa Sudan

cri

    Mjumbe wa serikali ya China, waziri msaidizi wa mambo ya nje Bwana Lu Guozeng leo amefanya ziara nchini Sudan, na kufanya mazungumzo na rais Omar el-Bashir wa Sudan na viongozi wengine wa nchi hiyo, wakibadilishana maoni kuhusu uhusiano wa nchi hizo mbili na suala la Darfur.

    Pande mbili zote zimeeleza kuridhishwa na maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, wakitumai kuwa nchi hizo mbili zitaimarisha zaidi ushirikiano katika sekta mbalimbali.

    Bwana Lu Guozeng ametoa pongezi kwa kusainiwa makubaliano ya amani kati ya pande mbili za Sudan. Akisema kuwa, serikali ya China inafuatilia sana mabadiliko ya hali ya Sudan, ikitumai kuwa pande husika zitafanya juhudi kwa pamoja ili suala la Darfur litatuliwe mapema.

    Viongozi wa Sudan wametoa shukrani kwa juhudi za serikali ya China katika utatuzi wa suala la Darfur, wakieleza kuwa, watajaribu kutatua suala hilo kwa njia ya kisiasa kadiri iwezekanavyo.