Umoja wa Afrika na Umoja wa uchumi wa nchi za Afrika ya magharibi(ECOWAS) tarehe 19 waliitaka tena serikali ya Togo kurudisha utaratiba wa katiba.
Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria, ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, alipokutana na ujumbe wa serikali ya Togo huko Abuja alisema kuwa, serikali ya Togo lazima irudishe utaratibu wa katiba uliokuwepo na rais Faure Gnassingbe anapaswa kujiuzulu kabla ya uchaguzi mkuu.
Katibu mkuu mtendaji wa ECOWAS Bw. Mohamed ibn Chambas alisema kuwa, kitendo cha Bw. Faure kurithi wadhifa wa urais hakilingani na katiba. Alisema Bw. Faure lazima ajiuzulu kabla ya uchaguzi mkuu, ama sivyo ECOWAS itaweka vikwazo kwa Togo.
|