Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-20 19:09:04    
New York-Bw. Kofi Annan atoa mwito wa kusuluhisha mgogoro unaohusika na katiba nchini Togo

cri

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan jana alitoa taarifa akitaka pande husika kusuluhisha mgogoro unaohusika na katiba nchini Togo kwenye msingi wa katiba na sheria.

    Alisema ameona kuwa Umoja wa Kiuchumi wa Nchi za Afrika ulianza kuiadhibu Togo na kusimamisha uanachama wake katika umoja huo kuanzia siku hiyo. Na alieleza wasiwasi wake kuhusu mazungumzo kati ya umoja huo na Togo kutoweza kupata maendeleo. Alisisitiza kuwa, pande husika lazima zichukue hatua za dharura ili kusuluhisha mgogoro huo kwa amani.

    Jana Rais Faure Gnassingbe aliviambia vyombo vya habari kuwa, serikali ya Togo inapenda kuioneshea jumuiya ya kimataifa kuwa serikali ya Togo "ina uwezo wa kulinda amani ya Togo".

    Baada ya rais wa zamani wa Togo Gnassingbe Eyadema kufariki dunia tarehe 5 mwezi huu, mtoto wake Faure aliapishwa kuwa rais wa Togo. Kutokana na sababu hiyo, makundi ya upinzani yalifanya maandamano yakimtaka kujiuzuru na kufanya uchaguzi huru na wazi. Umoja wa Afrika, Umoja wa Kiuchumi wa Nchi za Afrika na nchi kadha za Afrika pia zilitaka serikali ya Togo kufanya uchaguzi mkuu kwa wakati kufuatana na katiba.