Umoja wa uchumi wa nchi za Afrika ya magharibi ECOWAS, hivi karibuni umetangaza kuweka vikwazo kwa pande zote dhidi ya Togo ili kumlazimisha rais Faure Gnassingbe ajiuzulu. Wakati huo huo watu wa Togo walifanya maandamano makubwa mara kwa mara kwa kuiwekea serikali shinikizo kubwa zaidi. Hivi sasa serikali ya Togo inakumbwa na janga nchini na nje.
Tarehe 19 ECOWAS ilitoa taarifa ikisema kuwa rais Faure Gnassigbe wa Togo alitangaza kuwa nchi hiyo itafanya uchaguzi mkuu hivi karibuni, hatua hiyo bado iko mbali na ombi la umoja huo la kuitaka ifufue utaratibu wa katiba kwa pande zote, hivyo umoja huo umeamua kuiwekea vikwazo Togo. Vikwazo hivyo ni pamoja na kusimamisha kwa muda uanachama wa Togo katika umoja huo, kumwita balozi wa umoja huo kutoka nchini Togo, kupiga marufuku usafirishaji wa silaha kwa Togo na kuweka vizuizi vya utalii kwenye sehemu hiyo kwa viongozi wa serikali ya Togo na maofisa wengine wa nchi hiyo.
Tarehe 5 mwezi huu baada ya rais Gnassingbe Eyadema kufariki dunia kwa ugonjwa wa moyo, jeshi la Togo lilitangaza kumwachia mtoto wa rais huyo Faure ashike madaraka ya urais, baadaye bunge la Togo lilifanya marekebisho ya katiba, na Faure aliapishwa kuwa rais mpya.
Tokea hapo, nchi za Afrika na jumuiya ya kimataifa zilitoa taarifa kulaani hali ya Togo ya kukiuka katiba iliyokuwepo nchini humo, ambapo Umoja wa Afrika. ECOWAS na nchi kadhaa za Afrika zinaitaka serikali ya Togo ifufue mara moja utaratibu wa katiba uliokuwepo, na kufanya kwa wakati uchaguzi mkuu, ama sivyo zitaiwekea vikwazo.
Kutokana na shinikizo la kimataifa, Bwana Faure alirudi nyuma kidogo na kutangaza kuwa Togo itafanya uchaguzi mkuu ndani ya siku 60, lakini wakati huo alieleza kuwa, kabla ya uchaguzi mkuu, ataendelea kushika madaraka ya urais. Hatua hiyo imeufanya Umoja wa uchumi wa nchi za Afrika ya magharibi uamue kuiwekea vikwazo Togo. Baadaye Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Marekani na Ufaransa zilieleza kuunga mkono uamuzi wa Umoja wa uchumi wa nchi za Afrika ya magharibi, na kuifanya serikali ya Togo ajitumbukize katika hali ya upweke.
Vyombo vya habari vinaona kuwa, msimamo wa Umoja wa Afrika utafanya kazi muhimu kwa maendeleo ya hali ya Togo katika siku zijazo. Umoja wa Afrika uliwahi kusema kuwa, kama serikali ya Togo haitafuata katiba iliyokuwepo nchini humo, Umoja wa Afrika utaiwekea vikwazo pamoja na kusimamisha kwa muda uanachama wake. Hivi karibuni, msemaji wa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni rais wa Nigeria Bi Remi Oyo aliashiria tena kuwa, nchi za Afrika zinazoongozwa na Nigeria huenda zitachukua hatua zote pamoja na hatua ya kijeshi kuisaidia Togo kufufua utaratibu wa katiba. Kama Umoja wa Afrika ukiiwekea Togo vikwazo, serikali ya Togo itatengwa kabisa barani Afrika.
Hivi karibuni Umoja wa Ulaya pia ulitoa taarifa ikisema kuwa itasimamisha kwa muda kuzingatia kazi ya kufufua misaada yake ya uchumi kwa Togo.
Serikali ya Marekani tarehe 19 ilitangaza kusimamisha kwa muda mpango wake wa misaada ya kijeshi kwa Togo na kueleza kuwa itaangalia upya miradi yote ya kuisaidia Togo.
Wakati huo huo wapinzani wa Togo wanatumia fursa hiyo kuiwekea serikali shinikizo kubwa zaidi, na wamewahamasisha watu kufanya maandamano makubwa, walisema kuwa kila wiki watafanya hivyo, mpaka Bw Faure atakapojiuzulu.
Jumuiya ya kimataifa inafuatilia namna serikali ya Togo inavyokabiliana na janga la hivi sasa, na namna hali ya Togo inavyoendelea.
Idhaa ya Kiswahili 2004-02-21
|