Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-21 16:39:09    
"Urithi wa Kisiasa" wa Ariel Sharon

cri

Tarehe 20 vyombo vya habari vinaiita "Jumapili Maalumu", kwani katika siku hiyo baraza la mawaziri la Israel iliamua mambo mawili muhimu yanayohusu mpaka kati ya Israel na Palestina: Moja ni kuwa mpango wa upande mmoja umepitishwa na utaanza kutekelezwa kuanzia mwezi Julai mwaka huu; jingine ni kuwa ramani iliyorekebishwa ya "ukuta wa utenganishaji" imepitishwa. Vyombo vya habari vinaona kuwa, mambo hayo mawili yana maana ya kihistoria na yamedhihirisha wazi urithi wa kisiasa Bw. Sharon atakaoiachia Israel.

Tokea Desemba mwaka 2003 Ariel Sharon alipotoa mpango wa upande mmoja kwa lengo la kuwahamisha wakazi Wayahudi kutoka ukanda wa Gaza na sehemu ya ukingo wa magharibi wa Mto Jordan, sasa ameuvusha mpango wake kwenye kikwazo cha wapinzani, na amepiga hatua moja baada ya nyingine kuelekea kwenye lengo lake. Vyombo vya habari vinaona kuwa mambo yaliyopitishwa katika tarehe 20 yana maana kuwa mpango wa upande mmoja umevuka kikwazo cha mwisho na kupata haki ya kutekelezwa.

Kutokana na azimio lililopitishwa siku hiyo, serikali ya Israel itaanza rasmi kutekeleza mpango wa kuwahamisha wakazi Wayahudi, na mpango huo utatekelezwa katika vipindi vinne, na inatazamiwa kuwa utakamilika katika muda wa wiki 7 hadi 8 toka uanze kutekelezwa. Ingawa azimio linasema kuwa shughuli za uhamishaji za kila kipindi lazima zipate kibali kutoka baraza la mawaziri, lakini shughuli zenyewe haziathiri utekelezaji wa mpango.

Hata hivyo, hii haimaanishi hata kidogo kuwa Sharon anaweza kulala bila wasiwasi. Bajeti ya mwaka 2005 ambayo mpaka sasa haijapitishwa ni shinikizo kwa utekezaji wa mpango wa upande mmoja. Kutokana na katiba ya Israel kama bajeti iliyotolewa na bunge haitakuwa imepitishwa kabla ya tarehe 31 Machi, serikali ya Sharon itavunjwa, basi mpango wake utawekwa pembeni. Lakini vyombo vya habari vya Israel vinaona kuwa Sharon aliyetia uhai wa wake wa kisiasa kwenye mpango wake wa upande mmoja uliomfanya atumie juhudi zake za miaka mingi hatakubali kushindwa kutokana na bajeti hiyo.

Licha ya mpango wa upande mmoja kupitishwa, pia ramani iliyorekebishwa ya "ukuta wa utenganishaji" ilipitishwa kwa kura 20 dhidi ya moja. Tokea mpango wa kujenga "ukuta wa utenganisho" kutolewa ulikuwa unapingwa na jumuiya ya kimataifa kwa sababu ya kudhuru maslahi ya Wapalestina. Mahakama kuu ya Israel ilitoa hukumu ikitaka serikali ya Israel irekebishe ramani hiyo katika sehemu fulani. Baada ya ramani kurekebishwa inalingana zaidi na ile ya mwaka 1967 kabla ya kusimamisha vita vya tatu vya Mashariki ya Kati, lakini pia imekata kiasi cha 7% ya ardhi ya Palestina yenye Wapalestina elfu 10 kuwa upande wa Israel. Istoshe, ramani hiyo imevamia makazi ya ukingo wa magharibi wa Mto Jordan na makazi mengine ya Wayahudi kuwa upande wa Israel. Wachambuzi wanaona kuwa lengo hilo la Israel sio tu kuikalia sehemu ya ukingo wa magharibi ya Mto Jordan bali pia inaweka msingi wa kuimeza Jerusalem nzima baadaye, na kuzuia Wapalestina wasijenge nchi huru ya Palestina yenye mji mkuu katika sehemu ya mashariki ya Jerusalem.

Israel inasema kuwa ramani mpya ya "ukuta wa utenganishaji" imekubaliwa kimya kimya na Marekani. Kwenye barua Rais Bushi wa Marekani alisema kuwa Israel ina haki ya kumiliki makazi ya Wayahudi ya sehemu ya magharibi ya Mto Jordan. Palestina toka mwanzo ilikuwa na wasiwasi kuwa mpango wa upande mmoja ni ujanja wa Sharon kuacha maslahi madogo ili kupata maslahi makubwa kwa kuacha sehemu ya Gaza na kumeza ardhi kubwa yenye umuhimu wa kivita ya magharibi ya Mto Jordan na kuufanya "ukuta wa utenganishaji" kuwa mpaka kati ya Israel na Palestina. Ramani mpya ya "ukuta wa utenganishaji" iliyopitishwa tarehe 20 imethibitisha wasiwasi huo wa Palestina. Usiku wa tarehe 20 Chama cha Ukombozi cha Palestina kilitoa taarifa ikishutumu serikali ya Israel kuendelea kujenga ukuta na ikisisitiza kuwa ukuta huo umekwenda kinyume cha sheria husika ya kimataifa na pia "ramani ya njia ya amani" ya Mashariki ya Kati, na kwamba inataka jumuyia ya kimataifa na hasa Marekani iliingilie kati na kuzuia vitendo hivyo vilivyoathiri maslahi ya Wapalestina. Mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Mahmoud Abbas alipohojiwa na waandishi wa habari wa Ujerumani alisema, Israel haina haki ya kujenga makazi katika ardhi ya Palestina, na Marekani haina haki ya kuamua hatima ya Palestina.

Idhaa ya kiswahili 2005-02-21