Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-23 20:58:37    
Mazungumzo ya pande 6 ni njia mwafaka zaidi kuliko nyingine ya kutatua suala la nyuklia la peninsula ya Korea

cri

    Hivi karibuni mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea yamekuwa yakifuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. Tarehe 21 kiongozi mkuu wa Korea ya kaskazini Kim Jong Il alikutana na mkurugenzi wa Idara ya mawasiliano na nchi za nje ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bwana Wang Jiarui. Bwana Wang alifikisha ujumbe wa rais Hu Jintao wa China kwa Kim Jong Il.

    Katika ujumbe huo rais Hu Jintao alisema kuwa kupitia mazungumzo ya pande 6 ya kutatua suala la nyuklia na ufuatiliaji halali wa Korea ya kaskazini kunalingana na maslahi ya kimsingi ya China na Korea ya kaskazini, China inatumai kuzuia hali isizidi kuwa na utatanishi zaidi na kuanzisha tena mazungumzo ya pande 6. Kiongozi Kim Jong Il alisema kuwa, Korea ya kaskazini siku zote haipingi kufanya mazungumzo ya pande 6, na haitaki kujitoa kwenye mazungumzo hayo, kama baada ya juhudi za pamoja za pande husika, duru la 4 la mazungumzo hayo yakiandaliwa vizuri, Korea ya kaskazini itapenda kurudi kwenye mazungumzo hayo wakati wowote. Msimamo aliouonesha Kim Jong-il umewafanya watu waone matumaini ya kuanzishwa tena kwa mazungumzo hayo.

    Tarehe 10 mwezi huu, wizara ya mambo ya nje ya Korea ya kaskazini ilitoa taarifa ikisema kuwa serikali ya Marekani ingali bado ina jaribio la kuupindua utaratibu wa kisiasa wa Korea ya kaskazini, hivyo Korea ya kaskazini imelazimika kusimamisha kwa muda usio na kikomo kushiriki kwenye mazungumzo hayo. Hatua hiyo ya Korea ya kaskazini imefuatiliwa sana na pande mbalimbali katika siku za karibuni zilizopita, mawaziri wa mambo ya nje wa China, Marekani, Japan, Russia na Korea ya kusini waliongea kwa simu mara kwa mara kufanya majadiliano wakipendekeza kuendelea na mazungumzo ya pande 6 kwa kutatua suala la nyuklia la peninsula ya Korea.

    Mazungumzo ya pande 6 yanalenga kutatua ipasavyo suala la nyuklia la peninsula ya Korea na kuifanya sehemu ya peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na nyuklia, pande husika mbalimbali zote zinakubali lengo hilo. Hadi kufikia mwezi Juni mwaka jana, mazungumzo hayo yamefanyika kwa maduru matatu mjini Beijing, na kuanzisha majadiliano kuhusu masuala halisi, kubainisha zaidi lengo la kuifanya peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na nyuklia, kuthibitisha mwelekeo wa kufanya mazungumzo kwa kutatua suala la nyuklia na kutoa waraka wa kwanza tokea mazungumzo hayo yaanzishwe. Ukweli wa mambo umeonesha kuwa mazungumzo ya pande 6 ni njia mwafaka ya kutatua suala la nyuklia la peninsula ya Korea inayokubaliwa na pande mbalimbali.

    Lakini jambo linalostahili kutajwa ni kuwa, wakati wa kutafuta ufumbuzi wa suala la nyuklia la peninsula ya Korea pia lazima kuzinagatia na kutatua ufuatiliaji halali wa Korea ya kaskazini kuhusu usalama wake, hayo ni maoni ya pamoja kwenye mazungumzo ya pande 6. Na sababu kubwa ya kukwamishwa kwa mazungumzo hayo ni kuwa pande mbili za Marekani na Korea ya kaskazini zinakosa uaminifu kati yao. Marekani inaitaka Korea ya kaskazini "iache kwanza mpango wa nyuklia", na Korea ya kaskazini inaitaka Marekani ibadilishe kwanza sera yake ya uhasama dhidi yake.

    Kushikilia kuifanya sehemu ya peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na nyuklia na kulinda amani na utulivu wa peninsula hiyo kunasaidia amani ya Asia na dunia nzima. Hali ya hivi imeonesha kuwa msingi na masharti ya kurudisha mazungumzo bado upo, jumuiya ya kimataifa inatumai kuwa pande zote zinazohusika zitakuwa na uvumilivu, matarajio na imani ili kufanya juhudi kubwa kadiri ziwezavyo kwa ajili ya kurudisha tena mazungumzo ya pande 6 na kuhimiza utimizaji wa lengo la kuifanya peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na nyuklia.

Idhaa ya Kiswahili