Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-23 16:50:53    
China yaongoza duniani kwa uzalishaji wa ngano chotara

cri

    Baada ya jitihada za miaka zaidi ya 10, China imevumbua teknolojia ya uzalishaji wa "ngano chotara ya mfumo wa pili", ambayo hivi sasa imepandwa katika mashamba mengi nchini China.

    Kutokana na mpango wa utafiti wa miradi muhimu uliotangazwa na serikali ya Beijing tarehe 11 mwezi Januari, mkazo wa utafiti wa sayansi kuhusu "ngano chotara ya mfumo wa pili" umehamishiwa kwenye utafiti wa kimsingi na teknolojia muhimu. Katika miaka kadhaa iliyopita, chuo cha sayansi ya kilimo na misitu cha Beijing, ambacho kilibeba jukumu la utafiti wa "ngano chotara ya mfumo wa pili", kilipanda kwa majaribio ngano ya aina hiyo kwenye hekta 2,000 za mashamba, ambazo uzalishaji wake umeongezeka kwa asilimia 15.8 kuliko zamani na kufikia kilo 9,456 kwa hekta. Ngano ni zao kubwa la kwanza la kilimo duniani, hivi sasa duniani kuna teknolojia za kuua urithi wa ngano dume na ngano ya aina tatu ya mfumo wa 2, kati ya hizo hakimiliki ya "ngano chotara ya mfumo wa pili" ni haki ya China peke yake. Ikilinganishwa na teknolojia 2 za ngano chotara, ambazo hivi sasa bado zinaendelezwa katika maabara, ubora dhahiri wa "ngano chotara ya mfumo wa pili" ni kufanikiwa kupandwa katika maeneo makubwa na kuwa na ongezeko la uzalishaji katika kila hekta ya mashamba, ambapo nafasi ya China kuongoza katika utafiti wa ngano chotara duniani imethibitishwa.

    Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa teknolojia ya mradi wa ngano chotara cha Beijing Bw. Zhao Changping alisema kuwa "ngano chotara ya mfumo wa pili" ni yenye thamani kubwa ya kuenezwa. Aliongeza kuwa endapo nusu ya mashamba ya ngano yaliyoko nchini China yapatayo hekta milioni 26.6 kwa hivi sasa yakipandwa "ngano chotara ya mfumo wa pili", yatakuwa na ongezeko la pato la Yuan bilioni 2 na milioni 500, ikiwa tunafanya hesabu kwa kuwa na ongezeko la uzalishaji wa ngano kilo 750 kila hekta, China itakuwa na ongezeko la uzalishaji wa ngano kilo bilioni 10, ambazo zitaweza kutosheleza mahitaji ya chakula ya watu milioni 30 hadi 50. Bw. Zhao Changping alisema kuwa ngano chotara ni suala gumu duniani, ingawa baadhi ya nchi za nje zilianza kufanya utafiti kabla ya miaka 50 iliyopita, lakini hadi hivi sasa bado ngano hiyo haijaweza kupandwa katika maeneo makubwa. "Ngano chotara ya mfumo wa pili" si kama tuna inaweza kupandwa katika maeneo ya ukulima wa ngano hapa nchini, bali pia inaweza kulimwa katika maeneo yanayofanana duniani, hali ambayo itaweza kuimarisha nguvu ya ushindani ya China katika soko la mazao ya ngano duniani. Hivi sasa utafiti wa "ngano chotara ya mfumo wa pili" umethibitishwa na wataalam. Kutokana na kuungwa mkono na mtafiti wa taasisi ya utafiti wa uhandisi ya China Bw. Yuan Longping, kituo cha utafiti wa teknolojia ya mpunga chotara cha China kimekubaliana na chuo cha sayansi ya kilimo cha Beijing kuwa vitafanya utafiti kwa ushirikiano kuhusu tabia zinazofanana kati ya ngano chotara na mpunga chotara.

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-23