Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-23 21:26:55    
China inadhibiti kupatwa na suma ya Arsenic kutoka maji ya kunywa

cri

    Arsenic ni kemikali ya sumu kwa binadamu. Kwenye sehemu za vijijini magharibi na kaskazini mwa China, maji yaliyoko chini ya ardhi yana kiasi kikubwa cha kemikali hiyo, kunywa maji hayo kwa muda mrefu kunawafanya watu wa huko wapate ugonjwa wa arsenicosis na hata saratani. Tangu ugonjwa huo ugunduliwe kwa mara ya kwanza nchini China, serikali ya China imefanya juhudi katika kuboresha utaratibu wa utoaji wa maji ya kunywa kwenye sehemu hizo ili kupunguza madhara ya ugonjwa huo na kulinda afya za wakazi wa huko. waandishi wetu wa habari walifanya mahojiano maalum katika mkoa wa Shanxi ulioko kaskazini mwa China.

    Ugonjwa wa kupata sumu unaotokana na kunywa maji yenye kemikali ya arsenic una madhara makubwa kwa mwili wa binadamu, yakiwa ni pamoja na shinikizo kubwa la damu, kusababisha matatizo kwenye mshipa unaopeleka damu kwenye moyo na ubongo na baadhi ya magonjwa ya ngozi, na hata saratani ya maini na ngozi. Hivi karibuni, watu zaidi ya milioni 50 wanakabiliwa na ugonjwa huo kote duniani, na China ni nchi yenye wagonjwa wengi zaidi kuliko nchi nyingine duniani, maisha ya wachina milioni 3 yako hatarini kutokana na ugonjwa huo.

    Naibu mkuu wa idara ya kudhibiti magonjwa katika wizara ya afya ya China Bw. Xiao Dong lou alielezea hali ya kuenea kwa ugonjwa huo nchini China,

    "tangu ugonjwa huo ugunduliwe katika sehemu ya mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur mwanzoni mwa miaka ya 80, tumegundua ugonjwa huo kwenye mikoa ya Mongolia ya ndani, Shanxi na Jilin. Kati ya mikoa hiyo, hali ya ugonjwa huo katika mikoa wa Mongolia ya ndani na Shanxi ni mbaya zaidi na umeenea zaidi."

    Hivi karibuni, mbinu kubwa ya kukinga ugonjwa huo nchini China ni kuboresha miundo mbinu ya utoaji wa maji ya kunywa kwenye sehemu ambazo maji yaliyoko chini ya ardhi yana kiasi kikubwa cha kemikali ya Arsenic na kupunguza kiasi cha kemikali hiyo kwenye maji. Kuna njia mbili ya kuboresha miundombinu hiyo, kwanza kuchukua maji hukohuko na kupunguza kiasi cha kemikali kwa mbinu ya kikemikali; ya pili ni kuchukua maji safi katika mahali pengine na kusafirisha maji hayo kwenda kwenye eneo lenye ugonjwa huo.

    Mkoa wa Shanxi ulioko kaskazini mwa China ni moja ya mikoa inayoathiriwa vibaya na ugonjwa huo. Ili kuboresha miundombinu ya utoaji wa maji kwenye sehemu hiyo, kuanzia mwaka 2001 hadi sasa, serikali kuu ya China na serikali ya mkoa huo zilitenga fedha yuan zaidi ya milioni 100 kwa ajili ya mradi huo katika wilaya 18.

    Mwandishi wetu wa habari alitembelea mradi mmoja huko Fen yang mkoani Shanxi. Mradi huo ulichukua njia ya kusafirisha maji safi kutoka sehemu nyingine. Wahandisi waligundua chanzo kipya cha maji safi kwenye sehemu ya milima iliyoko kilomita 50 kutoka eneo la ugonjwa huo, na kusafirisha maji hayo hadi kwenye eneo hilo. Mkuu wa idara ya maji ya mji wa Fenyang Bw. Zhang Rong gui alieleza,

    "tulitenga yuan milioni 12 katika mradi wa kuboresha miundombinu ya utoaji wa maji mjini Fenyang, na tulichimba visima vinne vyenye kina cha mita 600 ambavyo vinaweza kutoa maji tani 6000 kwa siku. Hivi sasa maji hayo yanawatosheleza watu elfu 38 katika wilaya 2 na vijiji 21."

    Bw. Zhang Rong gui pia alieleza kuwa, kwa kuwa sehemu nyingi zinazotishiwa na ugonjwa huo ziko nyuma kiuchumi, mapato ya wakazi wa sehemu hizo ni madogo kuliko sehemu nyingine, hivyo bei ya maji baada ya mradi huo bado ni ya nafuu, yaani yuan 0.2 kwa tani, bei hiyo ni asilimia 5 hadi 10 ya bei ya maji katika miji, hali hiyo inapunguza mzigo kwa wakulima kwenye sehemu hizo.

    Bw. Yan Zhi xiang ni mkazi wa kijiji cha Xiao Jia Zhuang katika mji wa Fenyang, na kijiji hicho kimenufaika kutokana na mradi huo. alipohojiwa, alisema kuwa maji ya kunywa ya hivi sasa ni mazuri zaidi kuliko yale ya zamani,

    Mradi huo ulianzishwa mwaka 2001, na kabla ya hapo, wakazi wa hapa walikuwa wakipata magonjwa mara kwa mara, baada ya mradi huo kukamilika hali hiyo imebadilika. Hivi sasa tunaweza kunywa maji safi kwa bei nafuu."

    Mbali na mkoa wa Shanxi, mradi huo pia ulianzishwa kwenye sehemu nyingine zinazotishiwa na ugonjwa huo nchini China. ili kuimarisha zaidi kuunga mkono shughuli hiyo, mwaka 2002 serikali ya China ilitenga fedha yuan milioni 105 katika mradi huo.

    Ingawa fedha zilizotumika katika mradi huo zinaendelea kuongezeka, lakini kutokana na kuwa kuna sehemu nyingi zilizokumbwa na ugonjwa huo nchini China, hivyo hivi sasa kazi ya kukinga ugonjwa huo bado inakabiliwa na upungufu wa fedha. Kuhusu hali hiyo, naibu mkuu wa idara ya kudhibiti magonjwa ya wizara ya afya ya China Bw. Xiao Dong lou alisema,

    "China itaongeza nguvu na kutenga fedha nyingi zaidi katika kukinga ugonjwa huo, na kutarajia kutimiza lengo la kukamilisha mradi huo kwenye sehemu zote zenye maji yasiyo salamu ambazo zimegunduliwa mpaka sasa kabla ya mwaka 2006. Pia inapaswa kujenga mfumo wa kupima na kudhibiti hali ya ugonjwa huo ili kuweza kujua hali ya maendeleo ya ugonjwa huo."

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-23