Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-23 21:32:47    
Mapishi ya korosho pamoja na kamba-mwakaje

cri

Mahitaji

Kamba-mwakaje gramu 250, korosho gramu 100, ute wa yai, kiasi kidogo cha vitunguu maji, tangawizi, chumvi, M.S.G, wanga, maji ya wanga, supu ya kuku na mafuta.

Njia

1. Osha kamba-mwakaje, na wakaushe. Tia kamba-mwakaje ndani ya bakuli, tia chumvi, tangawizi, ute wa yai na wanga, kisha korogakoroga.

2. tia mafuta ndani ya sufuria mpaka yawe na joto la nyuzi 60 hivi, tia korosho ndani ya sufuria, mpaka rangi inapokuwa ya hudhurungi, na vipakue.

3. pasha moto tena, mpaka sufuria iwe na joto la nyuzi 40, tia kamba-mwakaje ndani ya sufuria, koroga na ipakue.

4. tia kiasi kidogo cha mafuta ndani ya sufuria, mpaka yachemke, mimina supu ya kuku, tia M.S.G, chumvi na maji ya wanga, chemsha, halafu, tia kamba-mwakaje na korosho, koroga na kupakua, kitoweo hiki sasa kiko tayari.