Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-24 19:21:50    
Uhusiano mzuri kati ya Marekani ya Ulaya hautarudi tena

cri

    Tarehe 22 viongozi wa nchi za NATO walifanya mkutano huko Brussels, viongozi wa nchi wanachama 26 akiwa ni pamoja na rais Bushi wa Marekani walihudhuria mkutano huo. Ni sawa kusema kwamba mkutano huo ulifikisha kileleni ziara ya Bw. Bush barani Ulaya. Rais Bush pia aliridhika na mkutano huo akisema kuwa uhusiano wa kando mbili za bahari ya Atlandiki kati ya Marekani na nchi za NATO unaweza kuaminika. Lakini watu wamegundua kuwa uchangamfu uliojaa katika mkutano huo hauwezi hata kidogo kuficha tofauti za ndani kati ya Marekani na Ulaya, na uhusiano kati ya pande mbili ni vigumu kurudi tena kama ulivyokuwa zamani.

    Miaka miwili iliyopita, Marekani ilianzisha vita dhidi ya Iraq bila kujali upinzani wa Ufaransa, Ujerumani na nchi nyingine za Umoja wa Ulaya, na ikasabisha tofauti kubwa isiyowahi kutokea kati ya Marekani na Ulaya tokea vita vya pili vya dunia. Ziara ya kwanza aliyochagua kuifanya barani Ulaya rais Bush baada ya kushika urais wa kipindi cha pili inadhihirisha tumaini la Marekani kutaka kurekebisha uhusiano huo. Ili kufanikisha na kuonesha jinsi alivyothamini ziara yake, rais Bush alituma huko waziri wake wa mambo ya nje Bi.Condoleeza Rice amtangulie na kufanya matayarisho. Urafiki uliooneshwa na Marekani, nchi za Ulaya pia ziliufurahia.

    Kwa sura mkutano huo ulifanyika katika hali ya maelewano mazuri, na uliafikiana katika masuala ya mapambano dhidi ya ugaidi, mafunzo kwa askari wa Iraq na masuala kuhusu amani ya Afghanistan na Mashariki ya Kati, lakini tofauti kati ya Marekani na Ulaya kuhusu masuala mengi muhimu ya kimataifa zinaendelea kuwepo. Kuhusu masuala ya Iran, hoja za kuanzisha vita dhidi ya Iraq na suala la kufuta vikwazo vya kuiuzia silaha dhidi ya China, misimamo ya pande mbili inagongana moja kwa moja. Kuhusu msimamo wa rais Bush kupinga kuondoa vikwazo vya silaha dhidhi ya China, rais wa Ufaransa Jacques Chirac alisema kinaganaga kuwa amri ya kuweka vikwazo vya silaha dhidhi ya China imepoteza hoja yake, kwa hiyo Umoja wa Ulaya unashikilia msimamo wa kufuta vikwazo hivyo.

    Tofauti kati ya Marekani na Ulaya pia zinaonesha kama muundo wa NATO utaendelea. Si muda mrefu uliopita, chansela wa Ujerumani alitangaza kuwa "NATO sio tena jukwaa la kwanza la nchi rafiki za kando mbili za bahari ya Atlantiki kujadili na kurekebisha sera". Wachambuzi wanasema kuwa usemi huo una maana uhusiano kati ya Marekani na Ulaya utakuwa wa mazungumzo ya usawa kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani, bali sio uhusiano uliovuka Atlantiki wa NATO. Kama msimamo huo utaitikiwa, utakuwa ni msiba kwa NATO. Ingawa mara moja Marekani ilipinga msimamo huo, lakini rais Chiraq wa Ufaransa unauunga mkono msimamo huo, na kwenye mkutano wa viongozi wa nchi za NATO rais huyo alisema, wazi uhusiano uliovuka bahari ya bahari ya Atlantiki lazima uzingatiwe kwani "mabadiliko yametokea barani Ulaya".

    Maneno kama hayo hakika rais Bush hayafurahi. Kwa kweli rais Busha anafahamu moyoni kwamba uhusiano kati ya Marekani ya Ulaya unazidi kuwa mbaya baada ya vita vya pili vya dunia, huu ni ukweli usiopingika. Tofauti kati ya Marekani na Ulaya ni tofauti ya kutetea upande mmoja tu na pande nyingi, au kwa maneno mengine ni tofauti kati ya upande mmoja unaotaka kuendelea na ubabe na upande mwingine utatetea dunia iwe yenye pande nyingi. Kwa uchambuzi wa mwisho tofauti hizo ni tofauti ya dhana za aina mbili na pia ni tofauti kati ya maslahi za aina mbili. Iwapo Marekani itashikilia ubabe kwa nchi za Ulaya, hakika itasababisha tofauti hizo kuzidi kuwa kubwa na kudhoofisha uhusiano wa sehemu hizo mbili.

    Ni sawa kwamba Marekani na nchi za Ulaya zina utamaduni wa namna moja na maslahi ya namna moja, itikadi yao ya namna moja ni kitu muhimu katika uhusiano wao. Katika siku za mbele uhusiano kati ya Marekani na Ulaya utaendelea katika njia yenye milima na mabonde.

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-24