Kundi la Chama cha ukombozi wa Palestina (FATAH), tarehe 23 usiku liliidhinisha orodha ya majina ya mawaziri wa baraza jipya la mawaziri iliyowasilishwa waziri mkuu Ahmed Qureia kwenye kamati ya utungaji wa sheria. Hatua hiyo inamaanisha kuwa huenda Bw. Ahmed Qureia anaweza kujinasua katika mgogoro wa uundaji wa baraza la serikali.
FATAH iliidhinisha orodha hiyo ya mawaziri kwenye mkutano ulioitishwa na kundi la wajumbe wa utungaji wa sheria kutoka FATAH siku hiyo usiku. Baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Palestina mwezi jana, mwenyekiti mpya wa mamlaka ya taifa ya Palestina Bw. Mahmmoud Abbas alimkabidhi Bw. Ahmed Qureia jukumu la kuunda serikali mpya kwa kufuata maagizo ya sheria za Palestina. Tarehe 21 mwezi huu, Bw. Ahmed Qureia aliwasilisha orodha ya majina ya mawaziri wapya kwenye kamati ya utungaji wa sheria. Miongoni mwa mawaziri hao 23, wanne ni wapya, ambao ni waziri wa mambo ya ndani Bw. Nasser Yusuf, waziri wa mambo ya nje Bw. Nasser al-Kidwa, waziri wa utalii Bw. Jed Ashak, na waziri wa mambo ya jamii Bw. Dalal Salameh, ambapo mawaziri wengine 19 kutoka kipindi kilichopita wanabaki kwenye nyadhifa zao za zamani au kupewa kazi mpya.
Orodha hiyo ya majina iliyotolewa na Bw. Ahmed Qureia ilipingwa na wajumbe wengi wa kamati ya utungaji wa sheria. Wanaona kuwa Palestina inahitaji mageuzi ya kisiasa ya kikamilifu ili kuboresha utawala na kutokomeza ufisadi, lakini katika orodha ya majina ya baraza jipya la serikali kuna mawaziri wengi wa zamani, na baadhi yao walituhumiwa kuhusika na vitendo ya ufisadi, ikiwa wataendelea kuwa mawaziri, hali hiyo itakwenda kinyume cha matarajio ya watu wa nchi hiyo. Baada ya hapo mwenyekiti wa kamati ya utungaji wa sheria Bw. Rawhi Fattouh alitangaza kuahirisha upigaji kura hadi tarehe 22.
Kutokana na shinikizo, tarehe 22 Bw. Ahmed Qureia alirudisha orodha ya majina ya baraza jipya la serikali na kutaka kamati ya utungaji wa sheria iahirishe upigaji kura kuhusu orodha ya majina ya baraza la serikali hadi tarehe 23. Bw. Qureia alisema kuwa atatumia watu wengi wapya kutokana na nia ya kamati ya utungaji wa sheria na kuanzisha serikali ya "mtindo wa wataalam". Habari zinasema kuwa katika orodha hiyo mpya, watu kumi ni wapya. Aidha, ni Bw. Nabil Shaath, ambaye amependekezwa kuwa naibu waziri mkuu na alikuwa waziri wa mambo ya nje, na waziri wa mambo ya mazungumzo Bw. Saeb Erekat walitoka kwenye kamati ya utungaji wa sheria, lakini 80% ya mawaziri katika orodha ya zamani walitoka kwenye kamati ya utungaji wa sheria. Endapo orodha hiyo mpya bado haitaweza kuridhisha wajumbe wengi wa kamati ya utungaji wa sheria, Bw. Qureia hana budi kuomba tena tarehe ya upigaji kura iahirishwe kwa siku moja kutokana na kushindwa kupata uungaji mkono wa watu wengi.
Wachambuzi wanaona kuwa kukabiliana kati ya Bw. Qureia na kamati ya utungaji wa sheria kuhusu suala la uundaji wa baraza jipya la serikali ni mvutano mkali kati ya kundi la wazee wa Palestina na kundi la viongozi vijana. Kiongozi wa kundi la viongozi vijana ambaye ni mshauri wa mambo ya usalama ya Palestina Bw. Jibril Rajoub ameshutumu Bw. Qureia kutojali madai ya mageuzi na kuleta mgogoro wa uundaji wa baraza jipya la mawaziri. Kiongozi mwingine wa kundi la viongozi vijana ambaye alikuwa waziri wa usalama wa zamani wa Palestina Bw. Mohammed Dahlan hivi karibuni alikataa kuchukua wadhifa wa katibu mkuu wa serikali ya Palestina kutokana na kupinga kwake orodha ya baraza jipya la mawaziri.
Sheria ya kimsingi ya Palestina inasema kuwa endapo orodha ya mawaziri wa baraza jipya la mawaziri iliyowasilishwa na waziri mkuu haitapitishwa katika upigaji kura wa kamati ya utungaji wa sheria, basi waziri mkuu anapaswa kujiuzulu. Katika wakati huo muhimu kundi hilo la FATAH katika kamati ya utungaji wa sheria liliitisha mkutano tarehe 23 usiku na kuidhinisha orodha ya majina iliyowasilishwa na Bw. Qureia siku hiyo hiyo. Kutokana na kuwa theluthi mbili za wajumbe wa kamati ya utungaji wa sheria walitoka FATAH, hivyo kuidhinishwa kwa orodha hiyo ya mawaziri wapya kwa kundi hilo la FATAH, kunamaanisha kuwa njia ya Bw. Qureia ya kutatua mgogoro wa uundaji wa baraza la mawaziri imepitika.
Wachambuzi wanasema kuwa hali hiyo inaonesha kuwa viongozi wa Palestina wanaweka mbele mambo makubwa ya Palestina na kushikilia umoja wa taifa.
Idhaa ya Kiswahili
|