Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-24 21:50:07    
Bendi ya muziki ya China "the flowers"

cri

Bendi ya muziki ya " the flowers" ilianzishwa mwezi Februali mwaka 1998, bendi hiyo ilipogunguliwa katika baa moja, wanamuziki wa bendi hiyo walikuwa bado wadofo ( Da Zhangwei miaka 14; Wang Wenbo miaka 15; Guo Yang miaka 19), hivyo bendi hiyo iliitwa " Bendi ya kwanza ya China iliyoundwa na watoto" na pia ilipewa jina la " bendi ya muziki ya vijana wenye kipaji". Mara bendi hiyo ilipojulikana katika eneo la muziki nchini China ilifuatiliwa na wataalamu wa muziki na vyombo vya habari. Mwezi Januari hadi Juni mwaka 1998, bendi hiyo ilipofanya maonesho ya muziki kwenye baa mbalimbali mjini Beijing, ilikaribishwa sana. Mwezi Septemba mwaka 1998 kampuni ya muziki ya Xinfeng ilianzishwa, hatimaye bendi hiyo ilisaini mkataba na kampuni hiyo, na kuingia kwenye fani ya muziki.

Tarehe 18 mwezi Januari mwaka 1999 bendi ya "The flowers" ilitoa albamu" furaha iko karibu". Albamu hiyo iliuzwa vizuri. ilijulikana kama ni " bendi ya muziki wa Rock & Roll yenye mustakabali mzuri" na " tumaini la muziki mpya kwa China". Mwezi Januari mwaka 2000, bendi ya "The flowers" ilifanya maonesho yake ya muziki kupitia kituo cha televisheni cha CCTV ambacho ni kituo kikubwa cha televisheni nchini China, bendi hiyo ilijulikana kwa watu wengi zaidi.

Kwa kuwa bendi hiyo ilichukuliwa kuwa msemaji wa vijana wa China, utetezi wake wa " Ukifikiri utafanikiwa" na " kuwaambia maoni yako", uliwapa vijana kumbukumbu kubwa. Wakati huo huo, katika sehemu mbalimbali za China, vijana walikuwa wanaanzisha bendi za muziki kwa kuiga bendi ya "The flowers", walichukuliwa bendi ya "The flowers" kuwa mfano wao wa kuigwa.

Hivi sasa wanamuziki wa bendi ya "The flowers" wamekuwa ni watu wazima, mbali na hayo bendi hiyo imekuwa na mwanamuziki mpya. Kuhusu siku za mbele walisema kuwa, wameshatunga mpango wa maendeleo ya siku za usoni lakini unatakiwa kutekelezwa kwa uwezo na nguvu zao zote.

wanamuziki wa Bendi ya muziki ya The flowers:

Da Zhangwei (umri wa miaka 22)-mwimbaji muhimu, mpigagitaa, mtunzi wa muziki na maneno ya wimbo;

Guo Yang ( umri wa miaka 27)- mpiga bass na anapenda kupiga picha;

Wang Wenbo ( umri wa miaka 23)- mpigagitaa, kinanda na mtunzi wa muziki na maneno ya wimbo;

Shi Xingyu ( mwanamuziki mpya )- mpigagitaa

Idhaa ya kiswahili 2005-02-24