Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-25 20:25:12    
Serikali ya mpito ya Somalia yapiga hatua ya kwanza kurudi nyumbani

cri

Rais wa muda wa Somalia Abdullahi Yusuf Ahmed na waziri mkuu wa serikali ya muda Ali Mohammed Ghedi tarehe 24 walirudi Somalia kutoka Nairobi, Kenya. Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wa serikali ya mpito ya Somalia kurudi nyumbani tangu kuanzishwa kwa serikali hiyo ya mpito huko Nairobi, Kenya mwaka jana.

Wakati Bwana Yusuf na Bwana Ghedi walipofika uwanja wa ndege wa Mogadishu, walikaribishwa na maelfu ya watu, na kupigiwa mizinga 21 ya heshima. Habari zinasema kuwa, ujumbe unaoongozwa na Bwana Yusuf na Bwana Ghedi una watu 47 wakiwemo mawaziri wanane na wabunge kadhaa, safari hii wanataka kukagua hali ya nchini Somalia na kutathimini kama hali ya hivi sasa inapevuka au la kwa kurudi nyumbani kwa serikali ya mpito na bunge la Somalia. Ujumbe huo unatazamiwa kukaa nchini humo kwa siku 10, ambapo utafanya ukaguzi katika miji 6.

Vyombo vya habari vinaona kuwa, kurudi Somalia kufanya ukaguzi kwa Bwana Yusuf na Bwana Ghedi kunaonesha kuwa serikali ya mpito ya Somalia imepiga hatua ya kwanza kurudi nyumbani, pia kunaonesha ukarabati wa nchi ya Somalia umeingia katika kipindi kipya.

Lakini wachambuzi wamedhihirisha pia kuwa, kutokana na hali ya Somalia ya kutokuwa na serikali imedumu kwa miaka 13, makundi mbalimbali yangali bado yana vikosi vyao vya kijeshi, tena miundo mbinu ya nchini humo imeharibiwa vibaya, hivyo kazi ya kurudi nyumbani kwa serikali ya mpito ya Somalia bado inakabiliwa na changamoto.

Kwanza mpaka hivi sasa bado haijathibitishwa sehemu iliko serikali ya mpito ya Somalia baada ya kurudi nyumbani. Ingawa serikali ya mpito imeanzishwa, lakini hali ya usalama wa mji mkuu Mogadishu bado ni ya wasiwasi, hata tokea mwaka huu matukio ya kuuawa kwa mkuu wa polisi na mwandishi wa habari yalitokea nchini humo. Na pia kuna migongano mikubwa kati ya watu wa ndani ya serikali ya mpito ya Somalia kuhusu kuifanya Mogadishu kuwa sehemu zitakapokuwepo idara za utawala wa serikali au la. Viongozi wa baadhi ya makundi wanapinga vikali kuifanya Mogadishu kuwa sehemu zitakapokuwepo idara za utawala wa serikali.

Aidha, bado kuna maoni tofauti kuhusu kupokea jeshi la ulinzi wa amani la nchi za nje kuisaidia serikali ya mpito ya Somalia kutuliza utaratibu. Kutokana na pendekezo la rais wa muda wa Somalia Bwana Yusuf, serikali ya mpito ya Somalia tarehe 5 mwezi huu iliuomba Umoja wa Afrika na Umoja wa nchi za kiarabu kutuma jeshi la ulinzi wa amani lenye askari 5000 hadi 7500 katika mji mkuu wa Somalia kwa mwaka mmoja, ili Somalia ijenge polisi na jeshi lake katika kipindi hicho. Ombi hilo limeitikiwa na Umoja wa Afrika. Lakini viongozi wa makundi fulani wa serikali ya mpito ya Somalia wanapinga pendekezo hilo, wanaona kuwa Somalia inaweza kukamilisha kazi ya kunyang'anya silaha kutoka kwa vikosi vya makundi, na kuanzisha polisi na jeshi lake bila kulindwa na majeshi kutoka nchi za nje.

Zaidi ya hayo, serikali ya mpito ya Somalia pia inakabiliwa na matatizo ya kifedha kwa kazi yake ya kurudi nyumbani. Katika hali hiyo, ni vigumu kuanzishwa kwa kazi ya kufufua miundo mbinu nchini na pia kuna athari ambayo haitasaidia kazi ya serikali ya mpito baada ya kurudi nyumbani.

Wachambuzi wamedhihirisha kuwa kutokana na taabu hizo, kazi ya kurudi nyumbani kwa idara zote za serikali ya mpito ya Somalia haiwezekani kukamilika katika muda mrefu. Makundi mbalimbali ya Somalia yakifuata kihalisi makubaliano ya amani yaliyofikiwa nchini Kenya na kutimiza ahadi zao, ndipo kazi ya ukarabati wa Somalia itakapoanzishwa bila vikwazo chini ya misaada ya jumuiya ya kimataifa.

Idhaa ya kiswahili 2005-02-25