Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-25 17:53:36    
Wachina washerehekea mwaka mpya wa Kichina nchini Sudan

cri

    Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya kasi ya uchumi wa China, makampuni mengi ya China yameanzisha shughuli zake katika nchi za nje. Mpaka hivi sasa, jumla ya makampuni 68 ya China yameanzisha matawi nchini Sudan barani Afrika. Makampuni hayo yanafanya shughuli katika sekta mbalimbali zikiwemo mafuta, biashara, ujenzi na afya, na idadi ya wafanyakazi wa China wanaofanya kazi kwenye matawi hayo nje ya China imefikia zaidi ya 5000, kati yao wengi wanafanya kazi katika kampuni za mafuta.

    Sikukuu ya Spring yaani sikukuu ya jadi ya mwaka mpya ya China ni sikukuu muhimu zaidi kwa wachina. Wakati wa sikukuu hiyo, wachina hupenda kusherehekea pamoja na jamaa na marafiki zao. Kila ifikapo sikukuu hiyo, wachina wanafanya shughuli mbalimbali za kusherehekea, kama vile matamasha, michezo na kuwatembelea marafiki. Lakini kwa wachina walioko nchi za nje, wanasherehekea vipi sikukuu hiyo muhimu kutokana na mila za kichina?

    Tarehe 8 mwezi Februari ilikuwa mkesha wa Sikukuu ya Spring ya mwaka 2005. Siku hiyo, kutokana na mwaliko wa balozi Zhang Dong wa China nchini Sudan, wajumbe wa makampuni mbalimbali wa China nchini Sudan walishiriki kwenye tamasha la kusherehekea Sikukuu ya Spring kwenye ubalozi wa China nchini Sudan. Ubalozi huo una eneo la mita 20,000 za mraba, eneo ambalo ni kubwa zaidi kuliko ubalozi wa nchi nyingine mbalimbali nchini humo. Hali ya kijiografia nchini Sudan inatofautiana na nchini China, mwezi Februari ni majira ya joto nchini Sudan, na maua na nyasi yanastawi kwenye ubalozi wa China, wachina ambao wamezoea kusherehekea Sikukuu ya Spring katika baridi walisherehekea sikukuu kwenye joto kali. Katika tamasha hilo kwenye ubalozi, wajumbe kutoka makampuni mbalimbali ya China walifanya maonesho ya michezo ya sanaa, ili kusherehekea sikukuu hiyo.

    Mbali na ubalozi, makampuni hayo ya China pia yaliandaa shughuli nyingi za kusherehekea sikukuu hiyo. Wafanyakazi wa China walisherehekea sikukuu hiyo kwa furaha kubwa nchini Sudan. Lakini kutokana na wasudan kutokuwa na sikukuu hiyo, wafanyakazi wengi wa China walipaswa kufanya kazi pia katika kipindi cha kusherehekea Sikukuu ya jadi ya mwaka mpya ya China.

    Kutokana na desturi ya China, watu hula chakula cha Jiaozi wakati wa mkesha wa Sikukuu ya Spring. Jiaozi ni chakula kinachotengenezwa kwa unga, mboga na nyama. Kati ya mboga za aina mbalimbali, liki (leek) ni mboga nzuri zaidi ya kutengeneza Jiaozi. Huko Khartoum mji mkuu wa Sudan, kuna mashamba 7 yanayomilikiwa na wachina. Kwenye mashamba hayo, wanapanda mboga za aina mbalimbali za kichina ambazo haziwezekani kupatikana kwenye soko nchini Sudan, mboga hizo haziuza kwa makampuni ya China nchini Sudan. Wakati wa sikukuu ya Spring, mboga ya liki ilihitajika sana, hata baadhi ya makampuni hayakuweza kupata ya kutosha. Lakini hayakuwa na wasiwasi, kwani mashamba hayo pia yalitoa mboga nyingine nyingi zinazoweza kutengeneza Jiaozi.

    Shamba la Zhongyuanyoutian lililoko umbali wa kilomita 20 kusini mwa Khartoum lilianzishwa mwaka 1989, ambalo pia ni shamba la wachina lililoanzishwa mapema zaidi nchini Sudan. Hivi sasa shamba hilo lina wafanyakazi watano wa China. Ili kutosheleza mahitaji ya wafanyakazi wachina wanaongezeka nchini Sudan. Shamba lake kuongeza maradufu eneo lake. Meneja wa shamba hilo Bw. Guo Shizhe alimwambia mwandishi wa habari kuwa, kila ifikapo Sikukuu ya Spring, shamba lake linakuwa na shughuli nyingi sana, kila siku linatoa mboga zaidi ya tani moja kwa makampuni ya China yaliyoko nchini Sudan. Hata wakati wa usiku baada ya wafanyakazi wa Sudan kuondoka kazini, wachina wanaendelea na kazi. Bw. Guo Shizhe anawapigia simu jamaa zake walioko nchini China kila wiki. Alieleza kuwa, hii ni mara yake ya pili kusherehekea Sikukuu ya Spring ya kichina nchini Sudan. Mwaka huu kabla ya Sikukuu ya Spring, kampuni kuu ya shamba la Zhongyuanyoutian nchini China lilimpeleka ofisa mmoja kuwatembelea wafanyakazi wake nchini Sudan. Baada ya kutembelea shamba hilo, ofisa huyo aliamua kuwajengea wafanyakazi hao wachina makazi mazuri zaidi, mbali na hayo aliwanunulia vifaa vya kisasa, ili waweze kutazama michezo ya China kwenye televisheni.

Idhaa ya Kiswahili 2005-02-25